0
Bango linalotahadharisha tatizo la Ukimwi nchini Afrika Kusini na wito kwa kupambana dhidi ya ugonjwa huo.

Vita dhidi ya Ebola visipelekei kusahau kupambana dhidi magonjwa yanayoathiri afya ya watu kama
ukimwi. Kufuatia siku ya kupiga vita dhidi ya ukimwi duniani, ripoti kadhaa zinaonyesha takwimu za kutia
moyo, ikiwa ni pamoja na ile ya milioni 15, kwa mfano.

Hii ni idadi ya watu ambao wanaweza kunufaika kutokana na matibabu katika mwaka 2015. Hata hivyo, vita dhidi ya VVU viko mbali kufaulu. 


Iwapo takwimu zinaonyesha maendeleo ya kweli katika mapambano dhidi ya Ukimwi, takwimu hizo huficha mara nyingi ukweli wa hali ya mambo.

Maambukizi mapya, ambayo ni takwimu muhimu kwa kupungua kwa Ugonjwa huo zimepungua kwa theluthi tatu tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000,
lakini pia kukosekana kwa usawa kunaonekana kuko juu.

 Katika nchi nyingi kusini mwa Sahara barani Afrika, lengo la kupunguza idadi ya maambukizi haliwezi kukamilika.
Uchunguzi wa mwaka huu unaonyesha kuwa dunia imefikia hatua ya mageuzi katika kufikia mwanzo wa
mwisho wa Ukimwi. 

Iwapo mafanikio makubwa
yamewezesha nchi 26 kupunguza nusu ya maambukizi yao mapya, wanapaswa kujua kwamba kwa upande mwingine, watu waliotengwa au kubaguliwa, wameendelea kushuhudia ongezeko la
maambukizi.

Ni vema kuelewa kwamba huduma bora pamoja na kufanya vipimo mara kwa mara bila kusahau kuendelea kupata tiba vinapaswa kupewa kipaumbele
Kaskazini na Kusini ili kukomesha maambukizi mapya kwa lengo la kupiga vita Ukimwi. 

Zoezi la kuhamasisha na kutoa taarifa kwa vijana wanaoishi kusini mwa Sahara barani Afrika linabakia kuwa
suala muhimu katika kupambana dhidi ya Ukimwi.

Tangu kuzuka kwa virusi vya Ebola vinavyoendelea kushuhudiwa Afrika Magharibi sekta ya Afya imeendelea kukabiliana na mdororo wa mfumo wa
matibabu , kwa sababu hata kama upatikanaji wa huduma bado unawezekana, wafanyakazi wa afya
kwa kiasi kikubwa wameathirika. 

Mbio dhidi ya muda zilianza ili janga la Ukimwi lisiendelei kupata nafasi
katika mataifa hayo.

Chapisha Maoni

 
Top