kuifundisha POLICE ya RWANDA ndiye
rasmi kocha wa Simba na atasaini
mkataba siku ya jumatano jioni.
Mserbia huyo atasaidiwa na kocha
kutoka Rwanda anaitwa JEAN MARIE
NTAGAWABILA .
Kocha Patrick Phiri amesema
ametaarifiwa kuhusiana na kibarua
chake kusitishwa.
Phiri raia wa Zambia amesema ni suala
la kawaida kumtokea kocha, hivyo hana
kinyongo na uongozi wa klabu hiyo.
"Wamenitaarifu kuhusiana na kuachishwa kazi, hili si jambo jipya, ingawa niliona tungeweza kubadilisha mambo.
"Najua Simba wanataka kufanya vizuri,
hivyo siwezi kumlaumu mtu na utaona
mwendo wa timu yetu ulivyokuwa,"
alisema Phiri.
Phiri amesema anasubiri kiasi cha fedha
alichokuwa anadai ambacho hakueleza
ni kiasi gani, halafu ataanza safari ya
kurejea kwao Zambia.
"Nikimalizana nao kuhusiana na malipo
yangu, nitajua lini ninakwenda nyumbani," alisema Phiri.
Chapisha Maoni