Watu kadhaa wanashikiliwa mateka na mtu mmoja au zaidi wenye silaha katika mgahawa wa Lindt mjini Sydney, Australia.
Mamia ya Polisi waliojihami kwa silaha
wamezingira eneo lilipotokea tukio hilo.
Takriban watu watatu wameonekana ndani ya mgahawa wakiwa wamenyanyua mikono juu wakiwa wameiegesha kwenye dirisha wakiwa
wameshika bendera nyeusi ikiwa na maandishi ya kiarabu.
Mmoja wa waliokuwa ndani ya mgahawa ambao uliovamiwa na watekaji nyara mjini Sydney
Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbot amesema tuki hilo linahuzunisha sana.
Abbot amesema haijajulikana nani alihusika na tukio hilo hata hivyo anahisi huenda ni njama za kisiasa na kuwa tayarikamati ya usalama ya taifa
imepewa taarifa.
Kamishna wa Polisi wa South Wales Andrew Scipione amesema tukio hilo halichukuliwi kuwa la kigaidi lakini imethibitishwa kuwa kuna mtu
mwenye silaha anayewashikilia mateka watu kadhaa.
Mashahidi wa tukio hilo wamesema walimuona mtu akiwa na begi na silaha akiingia kwenye mgahawa, polisi wamefunga eneo hilo, barabara na
kuwaondoa watu katika eneo hilo.
Chapisha Maoni