0
Chama cha wananchi CUF kimemtaka waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Hawa Ghasia kuachia ngazi kwa kusababisha vurugu katika
zoezi la kuapisha wenyeviti wa serikali za mitaa nchini.

CUF kimesema Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI kimechangia kwa kiasi kikubwa kuvurugika kwa zoezi la
kuwaapisha Wenyeviti wa serikali za mitaa jijini Dar es salaam kwa kuwaapisha viongozi ambao
hajashinda viti hivyo katika mitaa yao.

Akiongea jana jijini Dar es salaam Naibu Katibu Mkuu wa CUF kwa upande wa Bara Magdalena Sakaya amesema kuna baadhi ya mitaa ambako wagombea wa vyama vya upinzani wameshinda
na Serikali imewaapisha wagombea wa chama cha Mapinduzi CCM.

Akitolea mfano baadhi ya mitaa, Sakaya amesema hali hiyo imetokea katika mtaa wa Msisiri A Mwananyamala pamoja na mtaa wa Ukwamani Kawe katika manispaa ya Kinondoni Mhe. Sakaya amesema wananchi hawafurahishwi
na namna ambavyo serikali inawapa madaraka viongozi ambao hawajawachagua kuwaongoza
huku serikali ikitakiwa kutoa tamko kufuatia hali hiyo.

Chapisha Maoni

 
Top