HALI inazidi kuwa tete kwa vigogo kadhaa wa Serikali juu ya sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, baada ya kuwapo taarifa kuwa wengi watafikishwa mahakamani.
Iwapo leo vigogo ambao majina yao yamekuw yakitajwa tangu juzi watafikishwa mahakamani, wataongeza idadi baada ya juzi watumishi wawili
wa Serikali kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Jana asubuhi baadhi ya maofisa wa Taasisi y aKuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), walionekana wakiranda katika viwanja vya mahakama hiyo.
Mmoja wa maofisa hao alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya kuwapo kwao eneo hilo, alisema wapo kwenye maandalizi ya kuwapandisha
kizimbani vigogo wengine.
Hata hivyo, ilipotimu saa 7 za mchana, ofisa huyo alisema kuna baadhi ya nyaraka za watuhumiwa zilikuwa zinarekebishwa kabla ya kufika
mahakamani.
Baadhi ya watuhumiwa ambao jana walipigiwa simu na kutakiwa kufika Takukuru, inaelezwa hawakupokea simu kwa hofu ya kuburuzwa mahakamani. Hadi tunakwenda mitamboni
harakati hizo zilikuwa zimekwama.
Watumishi waliofikishwa mahakamani juzi ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Majunangoma ambaye alisomewa
mashtaka ya kupokea rushwa ya Sh milioni 323.4 zilizokuwa katika akaunti ya Tegeta Escrow kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engeering James Rugemalila.
Kabla ya Rugonzibwa kufanya kazi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alikuwa mwanasheria wa Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (RITA), ambako alihusika na mufilisi wa Kampuni ya IPTL.
Rugonzibwa, aliichunguza IPTL, alisimamia watumishi wake wakati kampuni hiyo iko katika mufilisi na alisimamia mashauri mbalimbali
yanayoihusu.
Mshitakiwa mwingine, ni Theophillo Bwakea ambaye alifikishwa mahakamani kwa kosa la kupokea rushwa ya Sh milioni 161.7 kutoka kwa Rugemalila.
Bwakea ni Mhandisi Mkuu wa Mradi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA), na kabla ya kufanya kazi huko, alikuwa Wizara ya Nishati na Madini, kitengo cha kusimamia umeme, ambako anadaiwa
alishiriki kutunga sera ya kampuni binafsi kuuza umeme Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na ilipoanza kutumika, Kampuni ya kufua umeme ya
IPTL ilikuwa ya kwanza kupata zabuni.
Ngeleja agoma Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, William
Ngeleja, amewagomea wajumbe wa kamati hiyo waliomtaka ajiuzulu kutokana na kutajwa kuhusika
na mgawo wa fedha za Escrow.
Pamoja na hatua hiyo, wajumbe walimtaka Ngeleja ajizulu au akae pembeni ili kumpisha makamu
mwenyekiti aongoze vikao jambo ambalo alilipinga.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu ambaye ni mjumbe kwenye
kamati hiyo, alisema tangu kuanza kwa vikao hivyo Januari 13, mwaka huu, Ngeleja amekuwa akiviendesha kwa nguvu licha ya wajumbe kumtaka akae pambeni.
“Amekuwa akiendesha vikao tangu juzi na hata juzi aliendesha na kuondoka saa 4 na kumwachia makamu wa kamati hii kumshikia,” alisema.
Alisema juzi baada ya Ngeleja kukaa na kuanza kuendesha kikao hicho, alimtaka kuachia kiti hicho kama ambavyo maazimio manane ya Bunge yalivyowataka wenyeviti waliotajwa kuhusika katika kashfa hiyo ya Tegeta Escrow ambapo yeye anadaiwa kupewa mgawo wa Sh bilioni 40.4
kinyume na sheria.
Lissu alisema pamoja na kumshauri kuachia ngazi, bado Ngeleja aligoma kwa madai akifanya hivyo ataonyesha wazi kuwa alihusika katika
kashfa hiyo.
“Ngeleja alisahau katika azimio la Bunge,
halikusema wale waliotuhumiwa walikuwa wezi, lakini akashindwa kujua katika azimio jingine Bunge lilitaka vyombo vya uchunguzi kuchunguza
ili watakaobainika wachukuliwe hatua ambazo zitathibitisha kama walihusika au la,” alisema Lissu.
Alisema sheria ya maadili ya uongozi wa umma, inawataka viongozi wa umma kutojihusisha na migongano ya kimaslahi na vitendo vya rushwa.
“Kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma, Ngeleja baada ya kutajwa katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), akihusishwa kupokea fedha hizo, ilitosha atangaze
kujiuzulu,” alisema Lissu.
Alisema kama Ngeleja, ataendelea kukiuka uamuzi wa Bunge, suala hilo watalirudisha bungeni ili lijadiliwe upya.
Zitto Akizungumzia kuhusu suala hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, alimsihi Ngeleja kutekeleza maamuzi ya Bunge kwa kuachia nafasi
hiyo.
“Namsihi Ngeleja kama kijana mwenzangu atekeleze maamuzi ya Bunge na aache kumtega Spika Anne Makinda,” alisema.
Nyumbani
»
HABARI
» Hali ni Tete kwa Vigogo
Escrow.......Wengine waliopata
Mgawo kupelekwa Mahakamani
leo
Related Posts
Tumuombee duwa njema mzee wetu Kig Majuto
Msanii maarufu wa maigizo Amr Athuman ‘King Majuto’ amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimb[...]
Aug 03, 2018Korea kaskazini kuchukua hatua
Korea kaskazini imesema itachukua hatua dhidi ya kutumwa kwa mfumo wa hali ya juu kuzuia [...]
Jul 11, 2016Shilingi bilioni 1.3 zakusanywa daraja la Nyerere
Jumla ya shilingi bilioni 1.3 zimekusanywa kutoka Daraja la Nyerere lililopo Kigamboni jijini Dar [...]
Jul 11, 2016RAIS MAGUFULI AMPOKEA WAZIRI MKUU WA INDIA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
1.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Waziri Mkuu wa India Na[...]
Jul 10, 2016Jeshi la Polisi Latoa ONYO Kali Kwa Vyama vya Siasa
ONYO limetolewa kwa vyama vya siasavinavyojaribu kusuguana na Jeshi la Polisikukumbuka kuwa hilo n[...]
Jul 10, 2016Haki sawa Wanawake walia Magufuli ‘kuwabania’ katika uteuzi
Mashirika yanayotetea haki za wanawake nausawa wa kijinsi nchini yamesema uteuzi wanafasi muhimu z[...]
Jul 10, 2016
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.