
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam, walisema suala la ndoa ni majaaliwa na si jambo unaloweza kupanga, kwa vile mwenye uwezo wa kufanya hayo yote ni Mungu, kama
ilivyo katika kuamua kuzaa au la.
Coletha Raymond ‘Koletha’, alisema katika maisha ya Kitanzania, wanaume ndiyo wenye uwezo wa kuamua. wataoa lini na ikawa kwa sababu wao
ndiyo wanaotongoza, lakini mwanamke hawezi kusema.
“Kuolewa natamani sana lakini bado sijapata mwanaume sahihi, naendelea kumuomba Mungu anipe, nawaomba na wengine wanisaidie kuomba,
kuhusu kuzaa niko tayari hata kama sijaolewa,” alisema.
Kauli kama hiyo ilitolewa pia na msanii wa filamu Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ aliyesema yupo tayari kuzaa hata kabla ya ndoa kwa sababu kuitwa
mama kwake ni muhimu kuliko ndoa.
Lakini katika hatua ya kushangaza, Baby Madaha ambaye pia anafanya muziki, alisema hana anachotamani kati ya ndoa wala mtoto, isipokuwa kitu muhimu kwake kwa sasa ni pesa.
“Katika maisha yangu sina mpango wa kuolewa wala kuzaa, ninachotafuta zaidi ni pesa na umaarufu, dunia nzima initambue, sijali cha umri wala nini, hayo ndiyo maamuzi ya maisha yangu.”
“Mimi siwezi kujua nitaolewa lini kwa sababu Mungu ndiye anajua ubavu wangu uko wapi na anakuja kwangu lini, pia siwezi kuwa na uhakika kama niliyenaye ndiyo ubavu wangu.
“Naweza nikasema naolewa mwaka huu kumbe nikaja kuolewa miaka miwili mbele. Suala la kuzaa kiukweli hakuna kitu natamani sasa hivi kama mtoto, hili sizungumzii sana, litakuwa ni sapraizi
kwa mashabiki zangu,” alisema Tamrina Poshi.
Kwa upande wake, Salma Jabu ‘Nisha’ alisema ndoa ni heshima kwa mwanamke, lakini anachoamini jambo jema hupangwa na Mungu.
“Mungu anatengeneza tutakayerandana na kupendana kiukweli na kuja kudumu kama wazee
wetu walivyokuwa, akimleta hata leo nitaolewa,”
alisema.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.