
Mpachika mabao huyo wa Ivory Coast, ambaye yupo na timu yake ya taifa kwa sasa kwa maandalizi ya Fainali za Mataifa ya Afrika, anajiunga na kikosi cha Manuel Pellegrini kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 25 huku
Pauni nyingine Milioni 3 zikiongezeka katika Mkataba huo wa zaidi ya miaka minne.
Bony, mwenye umri wa miaka 26, amekubali mkataba wa miaka minne na nusu na atakuwaanavalia jezi namba 14, ambayo awali ilikuwa
inavaliwa na Javi Garcia.




"Kama mchezaji wakati wote ni vizuri kuwa sehemu ya klabu kubwa duniani na ni fursa nzuri kwangu kuwa katika mazingira hayo – ninajivunia sana hilo,".
"Najisikia faraja sana kusubiri zama hizi mpya zifike, ni babu kubwa. Nafikiri ni uamuzi babu kubwa kwangu - Manchester City ipo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Unakumbuka mwishoni mwa msimu uliopita nilisema kwamba kama ninataka kuhama, itakuwa kwenye timu inayoshiriki mashindano hayo, kwa sababu ni michuano mikubwa ambayo ninataka haswa kucheza na kushinda pia,:.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.