
ulemavu wa ngozi – Alibinism, Pendo Emanuel akiwa hai au amekufa ikiwa ni pamoja na wahusika wa tukio hilo kukamatwa na kufikishwa
katika vyombo vya dola.
Agizo hili la mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, linakuja kufuatia watu wasiojulikana kumuiba mtoto Pendo Emanuel mwenye ulemavu wa ngozi majira ya saa 4 usiku Desemba 27
mwaka jana nyumbani kwao katika kijiji cha Ndami na kutoweka naye kusikojulikana, mkasa ambao umeilazimu kamati ya ulinzi na usalama
ya mkoa wa Mwanza kuapa kuwa serikali haitalala usingizi mpaka mtoto huyo mwenye umri wa miaka minne apatikane.
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi mkoa wa Mwanza Alfred Kapole amesema kuwa miongoni mwa kesi 72 zilizokuwa
mahakamani zikihusu mauaji ya walemavu wa ngozi, ni kesi tatu ndizo zilizotolewa hukumu mpaka sasa, huku akiilaumu ofisi ya mkemia mkuu wa serikali pamoja na mahakama kwa
kuchelewesha kesi hizo.
Mama mzazi wa mtoto Pendo, Bi. Sophia Juma pamoja na mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Chiriko Bi. Specioza Kasoli wamesema kila mtu ana haki ya kuishi na kulindwa na kuongeza kwamba mtoto huyo ni kati ya watu 74 wenye ulemavu wa ngozi wilayani
kwimba na alikuwa ni mtu wa 9 kwa kupatiwa ulinzi.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Valentino Mlowola amesema tayari askari polisi wamepiga kambi katika kijiji hicho kwa kazi moja tu ya kuhakikisha mtoto huyo anapatikana, lakini pia
watuhumiwa wanasakwa kwa udi na uvumba ili wafikishwe mahakamani kwa kosa la jinai.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.