0
Serikali mkoani Mwanza imesema hakuna kulala hadi mtoto Pendo Emmanuel (Albino) apatikane kufatia tukio la kutekwa kwaek na watu wasio julikana toka tarehe 27.12.2014 katika kijiji cha Ndami, Tarafa ya Mwamashimba Wilaya ya Kwimba
Mkoani Mwanza na kisha kutoweka naye kwenda kusiko julikana hadi sasa.

Mkuu wa Mkoa wa MWanza Mhe Magesa Mulongo, akiongea na wananchi wa kijiji hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo na kuwahusisha wananchi wakijiji hicho pamoja na uongozi wa Wilaya na Mkoa huku alitaka kujua hatua iliyofikiwa na wananchi hao katika kuwabaini waliofanya unyama huo.

Mtoto Pendo alitekwa na watu
wasiojulikana usiku wa tarehe 27.12.2014 majira ya saa nne usiku akiwa amelala na wazazi wake nyumbani kwao na kisha watekaji kutoweka naye na kwenda kusiko julikana hadi sasa.

Watu kumi na watano
(15), wanahikiliwa na jeshi la Polisi kwa
ajili ya mahojiano zaidi.
Akihutubia wananchi wa kijiji hicho Mkuu wa Mkoa wa Mwanza alisema ni tukio la kusikitisha kwani toka mwaka 2007 hakuna tukio la namna hiyo lililowahi kutokea katika Wilaya hiyo na tukio la mwisho lililotokea lilimkumba mwananchi wa Wilaya hiyo aliyekuwa amesafiri kwenda Mkoani Shinyanga kwa shughuli zake.

Amesema kiburi walichonacho watekaji
hakiwezi kuwa nje ya mipaka ya kijiji hicho cha Ndami bali mpango mzima unajulikana kwa wenyeji na ndio maana ilikuwa rahisi kufanya unyama huo.

“Kiburi cha watekaji kimo humu humu
haiwezekani mtu kutoka mbali aje atekeleze tukio hapa kijijini bila ya kuwa na wenyeji lazima kuna mtu au watu walioshirikiana na wahalifu hao”, alisema Mulongo na kuongeza “ kwa mazingira ya Nyumba ya
kina Pendo ilipo kule hakuna sehemu ya
kutokea na kama mliona pikipiki inaranda randa mchana,.. iweje mshindwe kuitilia shaka? Hapana, hii haikubaliki! mimi nimekuja kuwaambia nataka Pendo apatikane na sio vinginevyo, nawapa siku tano Ijumaa nitarudi hapa mniambie Pendo
yuko wapi! Alisema mkuu huyo wa Mkoa
akionesha kusononeshwa na tukio hilo.

“Mbona mifugo inapoibwa inapatikana”?
Aliwahoji viongozi wa sungu sungu na
kusema haiingii akilini kusema wakati wa tukio la utekaji sungu sungu wote walikuwa wamekwenda kula chakula na ndipo kadhia hiyo ilipotokea
Mkuu wa mkoa alihoji kufatia kauli
iliyotolewa na kiongozi wa sungusungu
kuwa wakati wa tukio askari wote wa
sungu sungu walikuwa wamekwenda kula majira ya saa tatu na tukio kutokea saa nne.

MWENYEKITI WA ALBINO MWANZA. Awali akielezea kusikitishwa kwake na tukio hilo, Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa Ngozi mkoani hapa Alfred Kapole, alisema inasikitisha kuona wanadamu wakiwauwa binadamu wenzao kama vile wanyama bila hata woga na vyombo vya maamuzi vikishindwa kutoa hukumu kwa wakati huku akielekeza lawama zake kwa mahakama na Mkemia
Mkuu.

“Mh. Mkuu wa mkoa inasikitisha kuona
miongoni mwa kesi 72 zilizokuwa
mahakamani, ni kesi 3 tu ndizo
zilizokwisha kutolewa hukumu” alisema
Kapole, na kuongeza ingekuwa ni kesi ya
wabunge wameshindana kwenye masuala ya uchaguzi ingekuwa imekwisha hukumiwa lakini kwa kuwa ni mlemavu wa ngozi, basi
kupuuzia kumekuwa kwingi mno",Alisema kapole.

Akinukuu maneno kutoka katika kitabu cha Biblia, Kapole alisema hata kama hukumu zitashindwa kutolewa na wanadamu hapa Duniani, naamini Mungu wa Mbinguni kuna siku haki itatendeka kwa kuwa
“Kitabu cha Mika 3.3-7 kinaeleza juu ya
hukumu watakayo ipata watu walao nyama za watu bila woga.

Kesi zinaendeshwa Polisi wanajitaihidi
sana lakini mkemia watendaji wa ofisi ya
mkemia mkuu wanatuhujumu kwa kuita
nywele zetu albino ni za Midoli, aling’aka
Kapole wakati akielezea kusikitishwa na
ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali pindi
inapo pelekewa Nywele.

Mwenyekiti Kapole pia aliomba kwa yeyote aliye na Mtoto huyo kumrejesha na kama wamemdhuru basi warejeshe hata mwili wake ili matanga yaweze kufanyika, akatumia fursa hiyo kumomba Rais wale
wote waliohukumiwa kunyongwa
wanyongwe ili kuepusha kuendelea kula
chakula cha serikali bure.

RC ITIKADI KATIKA KAZI. Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa aliwataka wanachi kuweka mbali itikadi zao za namna yoyote na kufanya kila linalowezekana ili kufanikisha zoezi zima la kuwasaka walio husika na utekaji
wa mtoto Pendo Emmanuel, ambao
unasimuliwa kuleta siamanzi kubwa ndani ya jamii ya wana Kwimba na watanzania lakini pia kuchafua taswira ya nchi mbele ya mataifa mengine ya Dunia . 

Huku akiwaonya watu wa haki za binadamu kuacha kupaza sauti za kuwatetea wahalifu. Tanzania inatajwa kuwa kinara cha ukatili huo tangu mauwaji hayo yalipo zuka mwanzoni mwa miaka ya 2006/2007.

TAKWIMU ZA KIMATAIFA.
Kwa Mujibu wa takwimu za kimataifa
zinaonesha ni asilimia 2% tu ya watu
ambao huzaliwa na ulemavu wa ngozi ndio hufikia na kusherekea miaka 40 ya
kuzaliwa kwao, huku pia takwimu
zikionesha katika nchi za Afrika mtu mmoja (1) kati ya elfu mbili (2000) huzaliwa wakiwa na ulemavu wa ngozi wakati katika marekani ni mtu mmoja kati ya elfu kumi na saba ndio huishi na ulemavu wa ngozi.

Mauaji ya Albino katika Tanzania
yanaonekana kushamiri katika Mikoa ya
kanda ya ziwa, ambapo imani za
kishirikina zikitajwa kuwa chanzo kikubwa cha mauwaji ya hayo lakini pia yale yalio wahusu vikongwe yanayo husishwa na masuala ya kujipatia utajiri wa haraka suala ambalo sio la kweli, ambapo takwimu zinaonesha kuwa mauwaji yalianza siku
nyingi japo kuripotiwa katika mamlaka za serikali na vyombo vya habari ilianza
mwaka 2006/2007.

Hivi sasa zipo asasi za kiraia zinazo
jihusisha na harakati za kupinga mauwaji hayo ikiwapo asasi ya Under The Same Sun ya Nchini Canada na kwa Tanzania imeshakuwa na tawi toka mwaka 2008.

KAMANDA WA POLISI.
Awali akitoa taarifa ya uchunguzi wa tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mulowola alisema tayari watu 15 wanashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoani humo kwa mahojiano zaidi akiwapo baba
mzazi wa Pendo, lakini pia jeshi hilo
limefanikiwa kuipata piki piki iliyotumika
kufanya unyama huo.

“Hivi sasa tunawashikilia watu wapatao
kumi na watano na wanaendelea kuhojiwa na Polisi” alisema Mlowola na kuongeza kuwa huo sio mwisho kwa kuwa jinai haina mwisho hata miaka ishirini tukio hili litaendelea kuchunguzwa”, na kusema hata
kama yeye atahamishwa au kustaafu kijana atakayekuja ataendelea na kesi hiyo, hivyo wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa kile wanacho kifahamu, alisema Mlowola na kusema tayari Jeshi hilo mkoani hapa limetangaza kutoa Milioni tatu 3 kwa atakayefanikisha kupatikana kwa mtoto Pendo.

Mtoto Pendo alikuwa ni miongoni mwa
alibino 74 waliopo katika wilaya ya
Kwimba na alikuwa namba 9 katika suala la kupatiwa ulizi. Imeandaliwa na Afisa habari Mwanza- Atley Kuni.
BW. ALFREDY KAPOLE MWENYEKITI WA
ALBINO MKOA WA MWANZA AKIZUNGUMZA KATIKA MKOA HUO.
WAANDISHI WA HABARI SHEILA SEZI NA GRACE CHILONGOLA WALIPOKUWA
WAKIONGEA NA MAMA YAKE NA PENDO.
NYUMBANI KWAO NA MTOTO PENDO,
MWENYEKITI WA ALBINO MKOA
WAMWANZA ALFREDY NA MWENYEKITI WA CHAWATA MKOA WAKIONGEA NA MAMA PENDO EMMENUEL.
 WANANCHI WA KIJIJI CHA NDAMI
WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA WA
MWANZA MAGESA MULONGO HAYUPO
HEWANI.

Chapisha Maoni

 
Top