WAZIRI wa Ujenzi Dkt. John Magufuli
ameagiza kufungwa kwa mfumo mpya wa kielektroniki katika vivuko vyote nchini ili kukabiana na wajanja wachache wanahujumu mapato katika vivuko hivyo.
Mbali ya hilo, ameagiza kufanywa kwa
utaratibu utakaowezesha huduma katika
vivuko zinatolewa kwa saa 24 ili kukidhi
mahitaji ya wananchi.
Dkt. Magufuli alitoa maagizo hayo jana
katika uzinduzi wa mfumo mpya wa
kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -
busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania.
"Tulianze pale Kigamboni na tukaona
mafanikio, tulipokuja hapa (Kigongo)
tukaboresha na mafanikio yameonekana
kwa kiasi kikubwa. Vivuko vyote sasa
vifungwe mfumo mpya wa
kielektroniki...vivuko vyote nchini," aliagiza Dkt. Magufuli.
Alisema mfumo huo una faida kubwa
ikiwemo kudhibiti upotevu wa mapato
ambapo katika kivuko cha kigongo - Busisi alisema mapato yameongezeka kwa takribani asilimia 40 baada ya kufungwa kwa mfumo huo.
Hata hivyo, Dkt. Magufuli alikataa kutaja
ni kwa shilingi ngapi mapato hayo
yameongezeka kwa hofu kuwa watu wenye dhmira mbaya wakisikia wanaweza kwenda na kufanya uhalifu.
Pia, aliagiza Kivuko kwa Kigamboni nacho kiboreshwe mfumo wake kama ilivyokuwa kwa Kigongo - Busisi. Waziri huyo wa Ujenzi, alisema kutokana na mafanikioyanayopatikana katika kudhibiti upotevu wa mapato na kurahisisha huduma kwa wananchi, wafanyakazi husika kwa maana
ya wale wa TEMESA maslahi yao
yanapaswa kuangaliwa upya na
kuboreshwa. "Kama mapato ni mazuri,
wafanyakazi nao walipwe vizuri, wasikae
kimasikini kwani wanapaswa kuona mwaka 2015 ni ukombozi katika maisha yao.
Alisema serikali chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete imefanikiwa kujenga madaraja yote makubwa nchini ambapo kwa sasa kuna madaraja 4880 nchini na kuwa wakati inapata uhuru kulikuwa na madaraja mawili ambayo yalikuwa ya kuvutwa.
Mfumo wa kielektroniki katika vivuko vya
Kigamboni na Kigongo Busisi ulifungwa na Kampuni ya Africom Tanzania ambaye Mkurugenzi Mtendaji wake Juma Rajabu alisema watahakikisha wanafunga mifumo ambayo itadhibiti upotevu wa mapato na kurahisisha huduma kwa wananchi ambao
ndiyo watumiaji.
Dkt. John Magufuli akikata utepe
kuzindua mfumo mpya wa kielektroniki
katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania.

Dkt. John Magufuli na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakifurahia baada ya kukata utepe kuzindua mfumo mpya wa

Mfanyakazi wa kivuko cha Kigongo -busisi mkoani Mwanza akionesha wananchi namna ya kutumia mashine hiyo.

Chapisha Maoni