0
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani
Kikwete akihutubia wananchi mjini
Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, Pwani,
ambapo pamoja na kuwashuru kwa
kumchagua, pia alisema atatumia
unasheria wake kuwasaidia wakazi wa
jimbo hilo wanaonyimwa haki zao za
msingi ikiwemo kuporwa ardhi.
 Ridhiwani akisisitiza jambo wakati wa
mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Masoko mjini Chalinze
Mkazi wa Chalinze, Bibi akitoa malalamiko yake mbele ya Mbunge Ridhiwani Kikwete ya kudhulumiwa shamba lake na watu wasiojulikana.
 Mkazi wa Chalinze Methodius Kaijage,
akiuliza swali kuhusu alama za x
zilizowekwa kwenye nyumba zao kwa ajili ya upanuzi wa barabara ambazo alidai ni takribani miaka kumi imepita bila kupewa fidia hivyo kusababisha kukosa maendeleo.
 Sehemu ya wakazi wa Kata ya Bwilingu,
wakiwa katika mkutano na mbunge wao
mjini Chalinze

Chapisha Maoni

 
Top