KIUNGO wa Cameroon, Alex Song amestaafu soka ya kimataifa baada ya kuachwa katika cha mwisho cha wachezaji 23 wa Simba Wasiofungika kwa ajili ya Fainali za Mataifa yaAfrika nchini Equatorial Guinea, ametangaza jana.
Song hayumo kwenye mipango ya kocha wa Cameroon, Volker Finke, ambaye amemdharau mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 tangu mwaka jana kwenye Kombe la Dunia Brazil ambako alitolewa kwa kadi nyekundu
baada ya kumchezea ‘kindava’ mshambuliaji wa Croatia, Mario Mandzukic wakifungwa 4-0 hatua ya makundi.
Song alifungiwa mechi tatu za kimataifa za mashindano na FIFA na licha ya kuwapo mazungumzo ya kuitwa baadaye kwenye kikosi cha Cameroon, mchezaji huyo anayecheza kwamkopo West Ham United kutoka Barcelona, ameamua kustaafu soka ya kimataifa. “Tangu Kombe la Dunia mwaka jana na kuenguliwa katika kikosi cha Cameroon cha Mataifa ya Afrika, nimeamua kustaafu soka ya
kimataifa,”amesema Song (pichani kushoto) , ambaye ameichezea timu ya taifa mechi 47.
“Ni kweli kulikuwa kuna majadiliano fulani ili niitwe baadaye kwenye kikosi kwa ajili ya mashindano haya, lakini nahisi baada ya majadiliano ya kina na familia yangu, huu ni uamuzi mzuri,”amesema katika taarifa yake
aliyoposti kwenye ukurasa wake wa Instagram.
“Mapenzi yangu kwa nchi yangu hayatabadilika, lakini nataka kutumia muda mwingi kuelekeza nguvu zangu katika ligi na kuanza kujijenga
upya West Ham United. Nawatakia kila la heri Cameroon na timu itabaki moyoni mwanguwakati wote,”.
Chapisha Maoni