Muhubiri wa kiislamu Abu Hamza aliyepewa kifungo cha maishaMhubiri wa kiislamu Abu Hamza amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa makosa ya ugaidi katika mahakama
moja mjini New York City.
Mhubiri huyo alifukuzwa nchini Uingereza mwaka 2012 kufuatia kesi ya muda mrefu na alipatikana na hatia miezi minne iliyopita.
Alipatikana na hatia katika mashtaka kadhaa ikiwemo njama ya kuwateka nyara watu kutoka nchi za magharibi ikiwemo Yemen mwaka 1998 na majaribio ya kuanzisha kituo cha mafunzo ya ugaidi kwenye jimbo la Oregon nchini Marekani.
Jaji alisema kuwa Abu Hamza alikuwa
amewachochea watu wengine kuwaua wale wasio waislamu kama jukumu la kidini na kusema kuwa alikuwa hatari kwa jamii.
Alifahamika kwa kutoa hotuba kali kwenye msikiti mmoja mjini London.
Chapisha Maoni