Mamia ya wanajeshi wanashika zamu mjini Paris baada ya siku tatu za ugaidi zilizouwa watu 17, huku taarifa zikitokeza kuhusu jinsi mfanyakazi Muislamu wa supermarket ya
Wayahudi mjini Paris alivyowaficha wateja 15 pamoja na mtoto mchanga wa mwezi mmoja wakati duka hilo liliposhambuliwa na gaidi.
Aliwaficha wateja kwenye chumba cha barafu. Lassana Bathily, kijana wa asili ya Mali, aliiambia televisheni ya Ufaransa kuwa aliwaongoza wateja
waliokuwa wamebabaika, hadi chumba cha chini kwa chini.
Alizima mtambo wa barafu na kuwaomba wakae kimya na alirudi juu dukani.
Baada ya duka hilo kukombolewa na askari wa usalama, Lassana Bathily alisema wateja walimshukuru kwa kunusuru maisha yao.
Chapisha Maoni