Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijiniDar,Kamanda Kova akitoa ufafanuzi wa
habari za taharuki katika vyombo vya
habari hususani televisheni,kuhusiana na sakata la kundi la Vijana wajiitao Panya Road,amesema suala hilo lilikuwa
dogo,lakini baadhi ya watu wamelikuza na kupelekea hofu kubwa kwa Wananchi ''Jiji mpaka sasa liko salama na wananchi watulie wasiwe na hofu kwa sababu jeshi la Polisi liko imara kuhakikisha amani inakuwepo ya kutosha,na hao vijana hawawezi kulishinda Jeshi la Polisi'',alisema.Alisema Wananchi waondoe hofu waendelee na shughuli zao kama kawaida.
Katika hali isiyo ya Kawaida na yakuogopesha,kumeibuka taharuki kubwa
usiku huu kwa Wakazi wa maeneo
mbalimabali ya jiji la
Dar,ikiwemo,Sinza,Kinondoni,Mwananyamala,Mabibo,Magomeni,Manzese,Kagera na Mburahati kwa kile kinachoelezwa kuwa vijana waitwao Panya Road wamevamia maeneo hayo na kuwajeruhi watu kwa vitu vyenye ncha kali,visu na mapanga na kuwapora vitu (mali zao) walivyokuwa navyo,kama vile haitoshi baadhi yao wamevunjiwa vioo vya magari yao.
Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa vijana hao waitwao Panya Roadwameibuka na kufanya uhalifu huo mara
baada ya tukio la Mwenzao mmoja kudaiwa kuuwawa na Polisi.
Aidha Chanzo hicho kimebainisha kuwa
baada ya taarifa kusambaa kwa
haraka,kimeeleza kuwa Jeshi la Polisi
limeingia kazini kuwasaka watuhumiwa
hao walioibua tafrani kubwa usiku huu.
Wadau tutazidi kuwaletea taarifa zaidi
kuhusiana na tukio hilo kadiri ya
zitakavyokuwa zikipatikana.
Chapisha Maoni