0
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akizunguza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya tume ya uchaguzi jijini Dar es salaam
wakati alipozungumzia maandalizi ya
uboreshaji wa daftari la wapiga kura, kura ya maoni ya Katiba mpya na uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu, kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Bw. Julius Mh.Julius Mallaba.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kutumia Bilioni 293 kwa ajili ya uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kwa mwaka huu ikiwa ni lengo kukuza demokrasia nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake jijini Dar es Salaam
leo ,Mwenyekiti wa Tume hiyo,Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema wamejipanga kuhakisha watu wenye sifa za kupiga kura wanajiandikisha ili waweze kupiga kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa pamoja na kupiga kura ya uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.

Lubuva alisema kuwa suala la kuwepo
wanajeshi katika uchaguzi , wataangalia
jinsi gani ya kufanya na kazi ya ulinzi
ibaki mikononi mwa jeshi la polisi.
‘’Suala la ulinzi wa jeshi tuliweke na
kuangalia jinsi gani tutafanya katika
kuhakikisha wananchi wanapiga kura kwa amani na usalama wa mali bila kuwa na hofu ya watu wanaowalinda’’alisema Jaji Mstaafu Damian Lubuva.

Aidha alisema uandikishaji wa majaribio,
utambuzi wa alama ya mpiga kura kwa
kifaa cha BVR ulikwenda vizuri na
mapungufu yaliyojitokeza wataendelea
kuboresha ili kila mtanzania aweze
kujiandikisha na kupiga kura.

Alisema uandikishaji wa kanda ya kwanza utaanza Februari 16 hadi Machi 15 ambapo hakutaja mikoa gani itaanza hivyo wanaandaa orodha ya mikoa na kanda katika jinsi ambavyo daftari la kudumu la mpiga litavyoweza kupita kuandikisha.

‘’Mambo yote yatakwenda sawa baada
kukamilika kwa daftari la mpiga kura
likiwemo upigaji kura ya maoni ya katiba
inayopendekezwa na maoni ya wadau
yataendelea kupokelewa katika ofisi
yetu’’alisema Jaji Lubuva

Chapisha Maoni

 
Top