0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Ijumaa, Januari 16, 2015, amekutana na kufanya mazungumzo na wajumbe wa Kamati Maalum Inayojitegemea Iliyofanya Tathmini ya Utekelezaji wa Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete amewashukuru wajumbe wa Kamati Maalum Inayojitegemea iliyofanya
tathmini ya utekelezaji wa Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete amewashukuru kwa kazi nzuri wajumbe hao saba wa Kamati hiyo ya BRN
Independent Review Panel ikiongozwa na Rais Mstaafu wa Botswana, Mheshimiwa Festus Mogae.

Wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni pamoja na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. James Adams, aliyekuwa Waziri katika Serikali ya Bwana Tony Blair ya Uingereza Lord Mandelson, Gavana wa Benki Kuu ya Botswana Bi.

Linah Mohohlo, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya ONE Bi. Sipho Moyo. Wengine ni Bwana Knut Kjaer kutoka Norway na Bwana Nkosana Moyo.

Wajumbe hao wamekutana kwa siku mbili kuanzisha juzi, Alhamisi, Januari 15, 2015 mjini Dar es Salaam ambako wametathmini mwaka wa kwanza wa utendaji wa BRN baada ya kuwa
wamepokea maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Presidential Delivery Bureau (PDB), mawaziri sita ambao wanaongoza sekta ambazo ziko katika
BRN kwa sasa na timu maalum ya Kampuni ya PWC ambayo ilifanya ukaguzi matokeo ya utendaji ya mwaka wa kwanza wa BRN.

Chapisha Maoni

 
Top