OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, imetoa siku nane kwa Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) Augustino Mrema kutoa maelezo kuhusu tuhuma za kuendesha chama
hicho kinyume na katiba.
Hayo yalibainishwa juzi katika taarifa iliyotolewa Dar es Salaam na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza ambayo ilimtaka kuwasilisha
maelezo yake kabla ya Januari 23, mwaka huu ili ofisi hiyo iweze kuyafanyia kazi na kuwajibu walalamikaji.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ukweli na Maridhiano TLP Taifa, Joram Kinanda, pamoja na Mrema kukiuka katiba ya chama chao, pia anatuhumiwa kuongoza chama kidikteta, kujilimbikizia madaraka na kuporomosha heshima
ya chama cha upinzani.
Kinanda aliongeza kuwa Mwenyekiti huyo, anaendesha chama hicho kwa ukabila kitu ambacho ni tofauti na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na ni tofauti na katiba ya chama chao.
Hata hivyo katika barua yake kwa Msajili, Kinanda aliiomba ofisi hiyo ifanyie kazi tuhuma hizo na kuruhusu Kamati ya Ukweli na Maridhiano kutambuliwa na kupewa mamlaka ya kuongoza
TLP kuelekea uchaguzi mkuu.
Pia aliomba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa itangaze kwamba Uongozi wa Mrema umekoma. Akifafanua kuhusu hatua hiyo, Nyahoza alisema kwa mujibu wa kanuni ya 13 ya kanuni za usajili
wa vyama vya siasa mlalamikiwa huyo atatakiwa kuwasilisha majibu ya tuhuma hizo kwenye ofisi yake siku iliyopangwa na sio zaidi ya hapo.
Related Posts
Sakata la Chadema na CCM BAVICHA wampinga Mbowe
Baraza la vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), limeapa kwenda mkoani Dodoma[...]
Jul 11, 2016Viongozi Watatu wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Watiwa mbaroni Mkoani Dodoma
JESHI la Polisi mkoani Dodoma linawashikiliaviongozi watatu wa Baraza la Vijana la Chamacha Demokr[...]
Jul 10, 2016Mtatiro Amtaka Profesa Lipumba Apumzike Uongozi
ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro amesema hana mpango wakugombea nafa[...]
Jul 10, 2016Lowassa Awapa Chadema Ukweli Kazi ya Chama cha Siasa ni Kukamata Dola na Sio Kupanga Maandamano
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassaamewataka viongozi wa Chama Cha Demokrasiana Maendeleo (Chade[...]
Jul 10, 2016Mvutano wa CCM na CHADEMA Walitikisa Jeshi la Polisi
Mvutano wa kisiasa baina ya vijana wa CCM na CHADEMA kuhusu katazo la mikutano ya vyama vya s[...]
Jul 08, 2016UKAWA tunajali maslahi ya Taifa kwanza
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Injinia James Fransis Mbatia amesema kwamba maamuzi yoyoteambayo k[...]
Jul 08, 2016
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.