WAKAZI wa kijiji cha Burunde kata ya Karitu wilayani Nzega mkoani Tabora, wamewapiga, kuwaua na kuwachoma moto watu watatu kwa tuhuma za kushiriki kumuua Helena Abel na
kumjeruhi mume wake, Said Msoma.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Juma Bwile alisema tukio hilo limetokea Januari 15 mwaka
huu.
Alisema kuwa Januari 12 mwaka huu Helena Abel na mume wake Said Msoma walivamiwa katika tukio hilo .Helena aliuawa na Said Msoma alifanikiwa kumjeruhi mmoja wa wahalifu hao
ambaye alikimbia.
Kamanda Juma alisema kuwa wananchi hao walifanya doria na kumkamata mhalifu huyo aliyejeruhiwa ambaye anaitwa Mainda Mahila na kuanza kumhoji kuhusika na mauaji hayo na
kukiri kufanya hivyo.
Bwile alisema kuwa mtuhumiwa huyo aliwaeleza wananchi hao kuwa mauaji hayo alifanya kwa kuagizwa na Mama Zainabu Hamis pamoja na mtoto wake aliyefahamika kwa jina la Zena
Yasoda.
Wananchi hao waliwapata watuhumiwa hao wawili kisha kuanza kuwapiga hadi kufa na baadaye kuwachoma moto.
Wakati huo huo mkazi mmoja wa kijiji cha Muhugi kata ya Muhugi wilayani hapa Chenge Kasinki (75) aliuawa na watu wasiofahamika baada ya
kuvamiwa nyumbani kwake.
Related Posts
Uchu wa madaraka chanjo cha vita vinavyoendelea Sudani Kusini
Ni nani aliyechochea mapigano ya karibuni huko Sudan Kusini yalioanza Ijumaa, Julai 8, yaliyosababis[...]
Jul 21, 2016Waziri Mkuu Aweka Jiwe La Msingi La Upanuzi Na Ukarabati Uwanja Wa Ndege Dodoma
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa mkoa wa Dodoma pamoja na Mamlaka ya Ustawishaji Maka[...]
Jul 21, 2016Dereva wa Basi la City Boy Asomewa mashitaka 30 ya Kuua
MMOJA wa madereva waliosababisha ajali ya mabasi ya City Boy Jumatatu iliyopita katika kijiji[...]
Jul 09, 2016Watoto Wanne wa Familia Moja Wateketea Kwa Moto Wakiwa Usingizini
HUZUNI imetanda katika wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, baada ya ajali ya moto wa kibatar[...]
Jul 09, 2016APOTEZA MAISHA KWA WIZI WA KUKU SENGEREMA
Mwanaume mmoja ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 mpaka 40 jina halijafahamika, [...]
Jul 08, 2016Weusi walaani mauaji Marekani
Hasira dhidi ya askari Polisi imezidi kuongezeka miongoni mwa watu wenye asili ya AFRIKA nchi[...]
Jul 08, 2016
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.