0
Rais Jakaya Kikwete amewaomba viongozi wa madhehebu ya dini kuendelea kuliombea taifa na watanzania kwa ujumla ili waweze kukabiliana na majukumu mengi na makubwa yaliyoko mbele yao kwa amani na utulivu likiwemo la kupata
katiba mpya.

Katika salam zake kwenye hafla ya kumsimika Askofu Solomon Masangwa wa Dayosisi ya Kaskazin Kati zilizowasilishwa na waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt Marry Nagu Rais
Kikwete amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa kuwawezesha viongozi wa dini kutimiza wajibu wao .

Akizungumza baada ya kusimikwa Askofu Solomon Masangwa amesema kazi kubwa aliyonayo ni kudumisha umoja na mshikamano na
kuendeleza yote yaliyoachwa na aliyekuwa Askofu wa Dayosisi hiyo marehemu Thomas Laizer.

Katika salam zao mkuu wa kanisa hilo nchini Askofu Dkt Alexs Malasusa aliyewawakilisha viongozi mbalimbali wa dini na waziri mkuu wa
zamani Edward Lowasa aliyewawakilisha viongozi
wa kisiasa wamewaomba waumini wa kanisa hilo na jamii kwa ujumla kudumisha ushirikiano na upendo miongoni mwao na kwa viongozi wao.

Katika hafla hiyo pia imehudhuriwa waziri mkuu mstaafu Fredrik Sumaye, Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Lazaro Nyalandu , wabunge, mabalozi na
maaskofu kutoka makanisa mbalimbali.

Chapisha Maoni

 
Top