0
Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakr Shekau.kundi hilo limedaiwa kuwateka vijana 40 katika kijiji cha Malari kazkazini mwa Nigeria


Takriban wavulana 40 na vijana wadogo
wameripotiwa kutekwa nyara na wapiganaji wa kundi la Boko haram Kazkazini mashariki mwa
Nigeria.

Wakaazi waliokitoroka kijiji cha Malari na kuwasili katika mji wa Maiduguri siku ya ijumaa usiku wanasema kuwa kitendo hicho kilitekelezwa siku
moja tu kabla ya mwaka mpya.

Wanasema kuwa watu waliojihami waliwasili katika kijiji hicho katika gari aina ya pick up na kuwaagiza wanaume wote kutoka nje ili kuweza
kusikiliza mahubiri.

Vijana wadogo baadaye walizungukwa na kupelekwa katika msitu jirani wa Sambisa. Mwaka uliopita kundi hilo la Boko haram liliwateka nyara zaidi ya wasichana 200 kutoka shule moja
ya bweni kazkazini mwa Nigeria.




Africa Newss
BBC

Chapisha Maoni

 
Top