shirikisho Afrika kati ya mabingwa wa Tanzania
Young Africans dhidi ya TP Mazembe mabingwa
wa DR Congo ukiwa ni mchezo wa pili kwa timu
zote mbili.
Mchezo huo umekuwa na mambo mengi sana nje
ya uwanja kitu ambacho kinazidi kuwafanya wadau
wengi wa soka la bongo kutamani kuona na hata
kujua ni nini kitatokea uwanjani ndani ya saa moja
na nusu ya mchezo huo (dakika 90).
Uongozi wa Yanga umetangaza kuwa hakutakuwa
na kiingilio kwenye game hiyo, sasa kilichotokea
ni kufurika kwa mashabiki uwanjani kuanzia
asubuhi wakianza kuingia uwanjani wakihofia
kukosa nafasi itakapofika majira ya mchana.
Africa Newss Sports imezinasa picha kadhaa huku
na kule na kukuletea wewe ili ujionee mwenye hali
ilivyo asubuhi hii na kama una mpango wa
kuushuhudia mchezo huo uwanjani basi utakuwa
unajua unatakiwa kufanya nini mida hii.
Chapisha Maoni