Chelsea wanajiandaa kuingia katika mbio za
kumwania kiungo wa Roma Axel Witsel, 27,
ambaye yuko Ufaransa na timu yake ya taifa ya
Ubelgiji katika Euro 2016 (Daily Mail), Barcelona
huenda wakamnyatia beki wa Arsenal Hector
Bellerin, 21, baada ya Dani Alves kuondona Barca
na kwenda Juventus (London Evening Standard),
Crystal Palace wamekubaliana ada ya uhamisho ya
pauni milioni 31.6 ya kumsajili mshambuliaji wa
Ubelgiji Mitchy Batshuayi, 22, anayechezea
Marseille (Guardian), Manchester City huenda
wakawazidi kete Manchester United na Benfica
katika kumsajili winga Marlos Moreno, 19,
anayeichezea Atletic Nacional ya Colombia kwa
pauni milioni 8 (Daily Mail), Real Madrid
wanapanga kumtoa mshambuliaji wake Jese, 23,
kwa mkopo msimu ujao, licha ya mchezaji huyo
kusakwa na Chelsea na Manchester United kwa
mkataba wa kudumu (AS), meneja wa Hull City
Steve Bruce anafikiria kumsajili mshambuliaji
kutoka Paraguay anayecheza Augsburg Raul
Bobadilla, 29, anayedhaniwa kuwa na thamani ya
pauni milioni 5 (Daily Mirror), Leicester City wapo
kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo
Nampalys Mendy, 24, kwa pauni milioni 13, kutoka
Nice (Leicester Mercury), Zlatan Ibrahimovic, 34,
atafanya vipimo vya afya Old Trafford wiki ijayo
kabla ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja (Sky
Sports), beki wa Chelsea Baba Rahman, 21,
anasakwa na Lazio ambao tayari wametoa dau la
pauni milioni 13 kumtaka mchezaji huyo wa
kimataifa wa Ghana aliyenunuliwa na Chelsea
msimu uliopita kwa pauni milioni 21.7 (Daily
Mirror), Napoli wamekubaliana maslahi binafsi na
Hector Herrera, 26, anayesakwa na Liverpool, lakini
klabu hiyo ya Italia bado haijakubaliana na Porto
ada ya uhamisho wa kiungo huyo (Tutto Mercatto),
Arsenal wamepanda dau kumtaka mshambuliaji
Gabriel Barbosa, 19, ambaye kifungu chake cha
uhamisho ni pauni milioni 40, katika klabu yake ya
Santos ya Brazil (ESPN Brazil), meneja wa Everton
Ronald Koeman anajiandaa kumsajili kipa Maarten
Stekelenburg, 33, ambaye alikuwa Southampton
msimu uliopita kwa mkopo akitokea Fulham
(Liverpool Echo).
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni