0
Manchester United wanakaribia kukamilisha
Dili za kuwasaini kuwasaini Kiungo
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Henrikh
Mkhitaryan na Zlatan Ibrahimovic.
Meneja Mpya wa Man United, Jose Mourinho,
anaisuka upya Timu yake na tayari
ashamchukua Beki wa Villareal Eric Bailly,
Mchezaji wa Kimataifa wa Ivory Coast.
Dortmund wamekuwa wakimng’ang’ania
Mkhitaryan aliebakiza Mwaka mmoja katika
Mkataba wake lakini sasa inaelekea Ofa ya
Pauni Milioni 30 ya Man United wataikubali.
Mkhitaryan, Raia wa Armenia, alijiunga na
Dortmund kutoka Shakhtar Donetsk Mwaka
2013 kwa Pauni milioni 23.5.
Dili hii inatarajiwa kukamilika ndani ya Wiki
moja.
Nae Zlatan Ibrahimovic, ambae pamoja na
Mkhitaryan Wakala wao ni mmoja, Mino
Raiola, tayari ana Makubaliano ya Awali na
Man United ikiwa pamoja na maafikiano ya
Mshahara wake, anatarajiwa kukutana na
Jose Mourinho Wiki hii.
Ibrahimovic ameondoka Paris St-Germain
hivi Juzi baada ya kumaliza Miaka Minne
ambapo alitwaa Ubingwa wa France mara 4
na sasa anatarajiwa kujiunga tena na Jose
Mourinho ambae walikuwa wote huko Inter
Milan Msimu wa 2008/09.
Hivi Juzi, Ibrahimovic, mwenye Miaka 34,
alitangaza kustaafu kuichezea Sweden
ambayo ilitupwa nje hatua ya Makundi ya
EURO 2016 bila yay eye kufunga hata Bao
moja.

Chapisha Maoni

 
Top