inaelekea ukingoni, sasa umebaki mchezo wa
fainali pekee kuhitimisha michuano hiyo, ambayo
kwa mwaka 2016 imefanyika maalum kusherekea
miaka 100 ya mashindano hayo toka yaanzishwe
1916.
June 26 2016 ilikuwa ni siku ambayo mchezo wa
kutafuta mshindi wa tatu ulichezwa kati ya
USA dhidi ya Colombia , kabla ya mchezo huo
Colombia alikuwa ana rekodi nzuri zaidi kuliko
USA , kwani walikuwa wamekutana jumla ya mechi
19, USA ameshinda mechi tatu kati ya hizo na
kupoteza 13.
Bado alfajiri ya June 26 iliendelea kuwa ngumu
kwa USA , kwani wamekuabli kupoteza mchezo wa
14 dhidi ya Colombia kwa kukubali kufungwa goli
1-0, goli ambalo lilifungwa na Carlos Bacca dakika
ya 31. Alfajiri ya June 27 ndio siku ambayo
utachezwa mchezo wa fainali utaozikutanisha
Argentina na Chile.
Chapisha Maoni