kuchukua uraia wa taifa lingine, baada ya
kuichezea Brazil kwenye michuano ya CONCACAF
Gold Cup mwaka 2003.
Thiago (33) alizaliwa kunako eneo la Sao
Bernardo do Campo, nchini Brazil. Aliichezea timu
ya taifa ya Brazil chini ya miaka 23, lakini
hakupata nafasi ya kujumuishwa kwenye kikosi
cha wakubwa.
Babu mzaa babu yake alikuwa ni raia wa Italy.
Mchezo wake wa kwanza kwa taifa la Italy ulikuwa
ni mwaka 2011, aliiwakilisha Italy kwenye
michuano ya Euro mwaka 2012 na Kombe la
Dunia mwaka 2014. Bado ni sehemu ya kikosi
cha Italy kinachoshiriki Michuano ya Euro mwaka
huu inayofanyika nchini Ufaransa.
7. Pepe (Brazil kwenda Ureno)
Pepe alizaliwa nchini Brazil lakini alihamia nchini
Ureno akiwa na umri wa miaka 18 kujiunga na
klabu ya C.S Maritimo.
Kamwe hajawahi kuitwa katika timu ya taifa ya
Brazil mpaka alipoamua kubadili uraia wake, lakini
kwa mujibu wa ripoti mbalimbali wakati fulani
Pepe alifuatwa na Dunga ili aweze kumwita katika
kikosi chake lakini alikataa kwa kuwa tayari
alikuwa ameshafanya maamuzi ambayo anahisi
yalikuwa sahihi.
6. Jonathan De Guzman (Canada kwenda
Uholanzi)
De Guzman alizaliwa nchini Canada huku baba
yake akiwa na asili ya Ufilipino na mama yake
Mjamaica.
Mchezaji huyo wa zamani wa Vallarreal alipata
makuzi yake nchini Canada mapaka alipofikisha
umri wa miaka 12, baadaye alihamia nchini
Uholanzi kujiunga na timu ya vijana ya
Feyernood.
Alikuwa na uhalali wote wa kuchezea Canada,
Ufilipino na na Jamaica lakini alichagua kuchezea
Uholanzi. Alifanikiwa kupata uraia mwaka 2008.
5. Neven Subotic (USA kwenda Serbia)
Beki huyu wa Dortmud aliazaliwa Yougoslavia, na
wazazi wenye asili ya Bosnia, alikuwa na uhalali
wa kuwakilisha taifa la Bosnia Herzegovina au
Serbia.
Wakati wa vita vya Serbia, familia yake ilihamia
Ujerumani halafu baadaye kwenda nchini
Marekani na kupata uraia wa nchi hiyo.
Akiwa kijana mdogo, Subotic alicheza klabu za
Sparta Gold na Impact Black. Hata hivyo aliamua
kuchagua kuchezea Serbia.
4. Miroslav Klose (Poland kwenda Ujerumani)
Huyu ni mfungaji bora wa muda wa muda wa
Michuano ya Kombe la Dunia. Alizaliwa Poland
lakini familia yake ilihamia nchini Ujerumani
wakati akiwa na umri wa miaka 8. Alikuwa na
uhuru wa kuchagua taifa lolote kati ya haya mawili
lakini kalamu yake ilidondokea kwa Ujerumani.
3. Kevin-Prince Boateng (Ujerumani kwenda
Ghana)
Kevin-Prince Boateng ni kaka wa mchezaji wa
Ujerumani Jerome Boateng. Baba yake alikuwa ni
raia wa Ghana wakati mama yake alikuwa ni
Mjerumani. Alipata makuzi yake nchini Ujerumani
na kuanza maisha yake ya soka katika klabu ya
Hertha BSC.
Amewahi kucheza timu za taifa za Ujerumani chini
ya Umri wa miaka 19 na 21. Lakini ilipofika wakati
wa kufanya maamuzi ya kuchezea timu ya
wakubwa, aliamua kuchagua Ghana.
2. Lukas Podolski (Poland kwenda Germany)
Lucas Podolski, ambaye kwa sasa anacheza
kunako klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki,
alizaliwa nchini Poland; na wazazi wake walihama
naye kwenda Ujerumani wakati akiwa na umri wa
miaka 2, na baadaye alianza kucheza mpira akiwa
na timu ya FC Koln mwaka 2003.
Kuna wakati aliomba kuchezea timu ya Poland
lakini kocha wa Poland kwa wakati huo Pawel
Janas alitilia shaka uwezo wake na kumpuuza.
Podolski baadaye aliamua kuchezea Ujerumani.
1. Diego Costa (Brazil kwenda Uhispania)
Straika wa Chelsea Diego Costa ni moja ya
wachezaji wanaochukiwa mno kwa sasa
ulimwenguni kutokana na utukutu wake uwanjani,
lakini vile vile kwa kupiga chini uraia wa timu
yake.
Costa (27) aliiwakilisha Brazil kwenye michezo
miwili tu ya kirafiki mwaka 2013, lakini aliomba
uraia wa Uhispania baadaye mwaka uliofuata
akapata fursa ya kuiwakilisha timu ta taifa ya
Uhispania kwenye michuano ya Kombe la Dunia
mwaka 2014.
Chapisha Maoni