wanakutana leo kujadili mustakabali wao wa
baadaye baada ya Uingereza kuamua kujiondoa
kutoka kwa muungano huo.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani,
ufaransa,Italy, Ubelgiji, Luxembourg na Uholanzi
wanatarajiwa kuanzisha mchakato huo pasi na
kuwa na ngoja ngoja.
Tayari rais wa tume ya muungano wa Ulaya ,
Jean-Claude Juncker, amesema anataka kuanzisha
majadiliano mara moja ya jinsi Uingereza
itakavyotoka rasmi kutoka EU .
Bw.Juncker amesema haieleweki kwamba swala
hilo likumbwe na hadi waziri mkuu wa Uingereza
David Cameron, ang'atuke kutoka madarakani
baada ya kushindwa katika kura hiyo ya maoni
iliyoamua nchi hiyo ijibandue kutoka Umoja wa
Ulaya.
Mawaziri hao pia wanatarajiwa kuweka masharti
mapya yatakayowazuia wanachama wengine kuiga
mfano wa Uingereza,baada ya vyama vya mrengo
wa kulia katika mataifa mengi duniani kupongeza
uamuzi huo wa Uingereza kujitoa kutoka
muungano wa Ulaya...
Hata hivyo waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani
Frank-Walter Steinmeier, amewatahadharisha
wenzake kutokuwa na hamaki na kutaka kuchua
hatua za kama kuilipizia kisasi Uingereza .
Ameomba kuwepo kwa subra na umakini katika
kulishughulikia swala hilo ambalo anasema
linapaswa kuongozwa tu na vipi kushughulikia
mahitaji ya raia wa jumuiya ya muungano wa
Ulaya.
Chapisha Maoni