Mgahawa huu waleta mapishi mapya ya
makange ya pweza, kamba (prawns) na
ngisi.
Samaki aina ya pweza amekuwa maarufu
sana hapa nchini Tanzania, kutokana na
ladha yake tamu na faida zake kiafya.
Kutokana na umaarufu huo vijana wa
kitanzania wameamua kuwa wabunifu
zaidi na kuanzisha mgahawa wa kisasa
maalum kwa ajili ya mapishi ya pweza,
kamba (prawns) na ngisi unaoitwa Pweza
Cafe .
Akiongea na mwanidishi wetu, mmoja wa
wamiliki wa mgahawa huo bwana Alfred
Kiwuyo alisema, "Sisi wenyewe ni wapenzi
wa supu na nyama ya pweza, kamba
(prawns) na ngisi lakini mazingira ya
awali ya kuuza vyakula hivi kwenye vituo
vya daladala na makutano ya barabara
kadhaa hapa jijini yalikuwa yanatukatisha
tamaa hasa ukizingatia usafi na mapishi
yenyewe haukuwa wa kuridhisha sana.
Sasa tukajiuliza swali je, haiwezekani kuwa
na sehemu ya kisasa zaidi ya kuuza pweza,
ngisi na kamba (prawns) na kukawa na
mapishi zaidi ya haya. Ndipo tukaamua
kuanzisha mgahawa huu ambapo tunapika
mpaka makange ya pweza, prawns (kamba)
na ngisi."
Muonekano wa Pweza Cafe kwa nje.
Vivyo hivyo akiongea na mwandishi wetu
mmoja wa wateja waliofika kwenye
mgahawa huo wa kipekee nchini alisema,
"Mimi nimekula makange ya pweza na ni
mara yangu ya kwanza na nimeyapenda
kwa kweli, ni matamu. Kwa mara ya
kwanza nilivyosikia makange ya pweza
nilishtuka kwanza nikasema lazima
niyaonje kwa kuwa tumezoea kula makange
ya kuku,ng'ombe, na mbuzi lakini sijawahi
kuonja makange ya pweza."
Watafiti wa masuala ya kiafya wanasema,
gramu 100 za nyama ya pweza ina madini
na vitamini za kutosha kwa mahitaji ya
mwili wa binadamu kwa siku. Kwa mfano
kiwango hiki cha nyama ya pweza
kinampatia mwanadamu mahitaji yake ya
siku ya madini ya chuma, seleniamu na
vitamini B-12. Madini haya na Vitamini hizi
ni muhimu katika kuusaidia mwili
kupambana na magonjwa,kutengeneza seli
hai nyekundu za damu na kuhakikisha
Chapisha Maoni