ZAIDI ya Sh milioni 800 zinatarajiwa kukusanywn na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti
Ukimwi (TACAIDS) kwa ajili ya kusaidia waathirikw wa Virusi Vya Ukimwi mwaka huu.
Fedha hizo zitakusanywa kupitia kampeni maalumu ya kupanda mlima Kilimanjaro ijulikanayo kama Kill Challenge inayofanyika kwa
mwaka wa 15, ambayo kwa mwaka huu wapanda mlima 100 wamejitokeza kushiriki.
“Mgodi wa Geita kwa kushirikiana na Tacaids unatarajia kupandisha watu 50 katika kilele cha mlima Kilimanjaro na kundi lingine la waendesha
baiskeli 50 linataraji kuzunguka mlima huo kwa
ajili ya kukusanya fedha hizo,” alisema Meneja Mawasiliano wa Mgodi wa GGM, Tenga Tenga.
Tenga alisema kampeni hiyo ya Kili Challenge inaongozwa na Balozi wake, Mrisho Mpoto ambaye ni msanii wa kughani mashairi na
upandaji huo wa mlima utafanyika Julai 16 na kumalizika Julai 22, mwaka huu.
Alisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, ambaye ataanzisha safari
hiyo huku mapokezi ya kuwapokea wapandaji hao
akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadiki.
Naye Mwakilishi wa Tacaids, Jackson Peter, alisema Kili Challenge ya mwaka huu imepata uzito wa kipekee kutokana na Umoja wa Mataifa
(UN) kupitia Shirika lake la Maendeleo la (UNDP)
kutoa wawakilishi wanane kushiriki upandaji
mlima huo kwa ajili ya kusaidia watu walioathirikn na Virusi Vya Ukimwi nchini.
Balozi wa Kili Challenge, Mpoto aliwataka wananchi na jamii kwa ujumla kutambua mapambano dhidi ya Ukimwi ni ya jamii yote hivyo inapaswa kuunga mkono jitihada za serikali
kwa ajili ya kupambana ili kufikia sifuri tatu.
“Naamini kwamba jitihada zinazofanywa na mfuko huu zinahitaji kuungwa mkono na Watanzania
wote na wadau wenye machungu na nchi hii,
hivyo tuungane kila mmoja wetu ama kwa
kuxchangia au kumuelisha mwenzake ili
mapambano haya yalete mabadiliko,” alisema
Mpoto.
Tangu kuanza kwa kampeni hiyo miaka 15
iliyopita zaidi ya Dola za Marekani 8,000
zimekusanywa na kugawiwa katika asasi
mbalimbali nchini zinazoshiriki katika
mapambano na kusaidia waathirika wa Ukimwi.
Fedha hizo zimepelekwa katika kusaidia
mapambano dhidi ya Ukimwi, ikiwamo kujenga
vituo vya ushauri na upimaji wa Ukimwi, ambavyo
baadhi yao ni vile vilivyopo mkoani Tanga,
Manyoni mkoani Singida na Geita.
Chapisha Maoni