0
Kituo cha kuvumbua na kuendeleza vipaji
vya muziki cha Mkubwa na Wanawe,
kimetoa msaada ya vifaa vya tiba na vifaa
mbalimbali vikiwe vile vya usafi, dawa za
meno, sabuni, maji na juisi kwa wodi ya
Watoto waliolazwa katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Jijini Dar es
Salaam.
Awali akizungumza wakati wa kukabidhi
vifaa hivyo, kiongoni wa kituo hicho, Said
Fella, amesema wameamua kufanya hivyo
kutokana na kuguswa na changamoto
zinazoikabili hospitali hiyo ya Temeke
ambayo pia ni majirani zao ambapo pia
amebainisha kuwa kundi hilo limekuwa
likifika Hospitalini hapo kuchangia
misaada mbalimbali.
Said Fella ameongeza kuwa, alishauriwa
na vijana wake waliopo katika kituo chake
kuona ni vipi wanaweza kushiriki katika
shughuli yoyote ya kijamii kwa kipindi hiki
cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa
Ramadhan na wote kwa pamoja
kukubaliana kutoa msaada huo.
“Nasi pia ni kama wagonjwa watarajiwa,
hivyo tumeona ni vema kuja kutoa msaada
wa vifaa mbalimbali vya tiba kama
tulivyoshauriwa na wenyeji wetu, tukiwa
pamoja na mabalozi wetu. Msaada tuliotoa
una thamani ya Sh milioni tatu,” alisema
Fella.
Akipokea msaada huo, mmoja wa
madaktari wa hospitali hiyo, Rashid
Nyumbiage, alikishukuru kituo hicho kwa
kuwakumbuka akiwataka wasanii na
viongozi wake pamoja na wengineo wenye
nafasi kuendelea kuwakumbuka.
“Vifaa tulivyoletewa ni Paso-Oximeter cha
kupimia kiwango cha oksijeni mwilini, HB
Culvate cha kupima kiwango cha damu,
mashine ya BP ambayo kazi yake ni
kufahamu kama presha ya damu (BP)
imeshuka au la na Mashine ya Nebulizer
yenye kazi ya kuwapimia dawa wagonjwa
wa pumu,” alisema Nyumbiage.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake
takribani 50 alioambatana nao hospitalini
hapo, msanii anayeunda kundi la Yamoto,
Dog Aslay, alisema kuwa wamefarijika
kuwasaidia wagonjwa akiahidi kufanya
hivyo wakati mwingine watakapopata
nafasi.
Tukio hilo la aina yake kwa kundi hilo
ambalo ufanya mara kwa mara katika
kutembelea jamii na kusaidia misaada,
limeweza kupongezwa na baadhi ya ndugu
wa wagonjwa na wagonjwa wenyewe kwa
kueleza kuwa ni tendo la kuigwa na kila
mmoja wetu hasa wasanii ambao ni kioo
cha jamii.

Chapisha Maoni

 
Top