0
Mwanamuziki kutoka Afrika Kusini, Black Coffee
ameshinda tuzo ya BET na kuwapiku mastaa
wengine saba walioteuliwa kuwania tuzo hiyo moja
tu Afrika akiwamo, Diamond Platnumz kutoka
Tanzania.
Diamond aliteuliwa kushiriki katika kipengere cha
‘Best International Act Afrika 2016’ kwa mara ya
pili, baada ya kushiriki mwaka mmoja uliopita
ambapo tuzo ilikwenda kwa Davido kutoka Nigeria.
Diamond alikuwa akichuana na baadhi ya mastaa
wa Afrika akiwamo Yemi Alade, Wizkid kutoka
Nigeria, maarufu ‘Black Coffee’ na Cassper
Nyovest wote kutoka Afrika Kusini, huku wengine
wakiwa ni Mzvee (Ghana) na Serge Beynaud (Cote
D’ivoire).
Hata hivyo, Diamond atafanya shoo katika jukwaa
hilo na itakuwa ni shoo ya kwanza kwake tangu
kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo
baada ya shoo hiyo, ametangaza ratiba ya shoo
zake zingine zinazofuatia.
Hii ni mara ya pili kwa Diamond kuteuliwa kuwania
tuzo hiyo kubwa duniani.

Chapisha Maoni

 
Top