haijapokea barua yoyote
kutoka Yanga wakiombwa
kumridhia beki Hassan Kessy
(pichani chini) aichezee
klabu hiyo.
Aidha, Simba SC imesema
haioni kwa nini mahasimu
wao wanasita kuandika barua
ya kuomba ridhaa ya
kumtumia mchezaji huyo,
ikiwa mwaka 1998
waliwaazima wachezaji
watatu, beki Alphonce
Modest, kiungo Shaaban
Ramadhani na mshambuliaji
Monja Liseki.
Taarifa zaidi ya Simba
iliyotolewa leo kwa vyombo
vya Habari inasema; "Awali
ya yote klabu inaendelea
kutoa pongezi kwa ndugu
zetu waislaam wanaoendelea
kufunga mwezi mtukufu wa
Ramadhani tunaamini
Mwenyezi Mungu atawalipa
malipo mema kwa ibada hiyo
muhimu.
Ndugu wanahabari katika
siku za karibuni hususan
kuelekea mchezo wa Yanga
na klabu kutoka Congo DRC
TP Mazembe Englebert
kumekuwa na maneno mengi
kutoka klabu ya Yanga
yakiishutumu klabu yetu
kuhusiana na kutokutoa
ruhusa kwa mchezaji Hassan
Ramadhani 'Kessy' na pia
kuhusiana na namna
mashabiki watakavyokaa
majukwaani siku ya mchezo
huo jumanne ya wiki hii.
Klabu ya Simba kwa maksudi
kabisa inapenda kutoa
ufafanuzi kuhusiana na
mambo hayo mawili
yanayoleta sintofahamu
miongoni mwa wadau wa
mchezo huu murua wa
kandanda.
Hakuna barua yoyote
ambayo klabu ya Yanga
imetuandikia kuhusiana na
suala la mchezaji Hassan
Ramadhani 'Kessy' pia
hakuna hata mazungumzo
yaliyofanyika baina ya
viongozi wa vilabu hivi ili
kutuomba walau kwa mdomo
kama taratibu zinavyotaka.
Ikumbukwe Simba huwa
haina tatizo kuruhusu
matakwa binafsi ya mchezaji
na nyote mnajua utamaduni
huo wa klabu yetu.
Kwa wasiofahamu mwaka
1998 klabu ya Simba
iliwaazima wachezaji watatu
Yanga ili wacheze hatua ya
makundi kama hii ya klabu
bingwa Afrika wachezaji hao
ni Shaban Ramadhani Monja
Liseki na Alphonse Modest
sasa jiulize kama tuliweza
kuwaazima wachezaji vipi
tushindwe kumruhusu
mchezaji waliyemsaini?
pamoja na maneno yao ya
kuudhi Simba ni waungwana
wa kutosha na wao
wasitumie ukimya wetu
kuwapotosha wanachama na
washabiki wao eti
tumewakatalia kuwajibu
barua ya Hassan Ramadhani
'kessy'
Msimamo wetu kuhusiana na
jambo hili inategemea
uungwana wao tu.
Pia Yanga kupitia msemaji
wao wamenukuliwa kuwa
kwenye mchezo dhidi ya TP
Mazembe watakaa kwenye
majukwaa yote hata yale
ambayo kwa utamaduni wa
uwanja wa taifa hukaliwa na
mashabiki wa klabu yetu.
Tunafahamu kuwa kauli hii
ina nia ya kuchochea vurugu
kubwa kwenye mchezo huo
na sote tunajua athari ya
vurugu michezoni
tunawashauri Yanga
wasijaribu kuleta mashabiki
wao kwenye majukwaa
wanayokaa washabiki wa
Simba ili kuleta amani siku
hyo ya mchezo.matarajio
yetu vyombo vinavyohusika
vitasimamia kwa ukaribu
jambo hilo.
Mwisho ingawa si kwa
umuhimu klabu haimzuii
yoyote kushangilia timu
yoyote siku ya mchezo huo
kama zilivyo desturi ya wao
Yanga kushangilia klabu
yoyote inayocheza na Simba
hususan wageni toka
nje.kama ilivyokuwa miaka
michache nyuma ambapo
walishangilia na kuvaa jezi za
TP Mazembe.
Waarabu wana msemo wao
maarufu "KAMA TUDINI
TUDANI" kama ulivyofanya
na wewe utafanyiwa hivyo
hivyo," imemalizia taarifa
hiyo.
(Imetolewa na Haji Sunday
Manara, Mkuu wa Idara ya
Habari na
Mawasiliano, Simba Sports
Club)
Chapisha Maoni