Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, staa wa filamu
Bongo, Irene Uwoya juzikati alimtia majaribuni
msanii mwenzake Single Mtambalike ‘Richie’
walipokuwa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee
jijini Dar kulikokuwa na harusi ya mdogo wake
Steve Mengere ‘Steve Nyerere’, Happy Mengere.
Irene Uwoya na Richie.
Kwenye ‘mnuso’ huo, Uwoya aliyekuwa amevalia
kivazi kilichoacha mapaja yake wazi, alionekana
mara kadhaa akimkumbatia Richie na hata
paparazi wetu alipotaka kuwafutoa picha, staa
huyo alimshika kimahaba na kuwaacha watu
wakinong’ona chinichini.
“Uwoya hivi haoni anamtia mwenzake
majaribuni? Na Mwezi Mtukufu huu analazimisha
kupiga naye picha ya kumkumbatia, ila hawa
wasanii wamezoeana sana,” alisema mmoja wa
waalikwa aliyekuwa karibu na mastaa.
Irene Uwoya na Richie.
Paparazi wetu aliyekuwa eneo la tukio alipojaribu
kuwakaribia na kumuuliza Uwoya kulikoni
anamfanyia mwenzake vituko alisema, alijisahau
kuwa Richie yupo kwenye Mwezi Mtukufu ila
alipiga picha hiyo kama pozi la kawaida tu na
wala hakuwa na nia mbaya.
Chapisha Maoni