0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Juni, 2016 amewaapisha wakuu wa Mikoa watatu
aliowateua Jumapili iliyopita tarehe 26 Juni, 2016.
Wakuu wa Mikoa walioapishwa leo Ikulu
Jijini Dar es salaam ni Dkt. Binilith Satano
Mahenge ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma, Dkt. Charles Ogesa Mlingwa
ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mara na Bi.
Zainab Rajab Telack ambaye ni Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga.
Hafla ya kuapishwa kwa wakuu hao wa
Mikoa imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, wakuu wa
vyombo vya ulinzi na usalama na wakuu wa wilaya wateule ambao waliteuliwa na Rais Magufuli Jumapili iliyopita tarehe 26 Juni, 2016.
Aidha, miongoni mwa wakuu wa wilaya 139
walioteuliwa, Rais Dkt. John Pombe
Magufuli amefanya mabadiliko madogo
katika wilaya tatu ambapo ametengua
uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mteule Mhe. Fatma Hassan Toufiq na badala yake
amemteua Bi. Agness Elias Hokororo kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, ametengua uteuzi wa
Mkuu wa wilaya ya Serengeti Mteule Bw.
Emile Yotham Ntakamulenga na badala yake amemteua Bw. Nurdin Hassan Babu kuwa
Mkuu wa Wilaya hiyo na ametengua uteuzw wa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mteule Bw.
Fikiri Avias Said na badala yake amemteuB Bw. Miraji Mtaturu kuwa Mkuu wa wilaya
hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli amewataka wakuu wa
wilaya wateule kwenda kuchapa kazi na
kutatua kero za wananchi katika wilaya zao
huku wakizingatia kufanya kazi kwa
uadilifu na uaminifu.
Rais Magufuli pia amewataka kusimamia
ukusanyaji mapato ya serikali na matumizi
ya fedha na rasilimali nyingine za umma,
kuhakikisha wananchi wapo salama na pia
kuhakikisha wananchi wanafanya kazi za uzalishaji mali.
"Katika kazi hizi wapo watakaowakejeli,
katika kazi hizi wapo watakaowadhihaki,
nyinyi kavumilieni na mmuweke Mungu
mbele na mkawaweke watanzania mbele, mkafanye kazi kadiri Mungu atakavyokuwa
amewaongoza.
"Nataka kuwahakikishia tunawaunga
mkono kwa nguvu zote, mkafanye kazi bila
uwoga wowote, katembeeni kifua mbele, kwa sababu tumewaamini wala msiwe na wasiwasi, ukifanya kitu kizuri kwa dhamirabyako iliyo njema kitazaa matunda mazuri,
ukifanya kitu kwa unafiki hakitafanikiwa"
Amesema Rais Magufuli.
Katika hafla hiyo, wakuu wa mikoa
walioapishwa na wakuu wa wilaya wateule wamekula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa
viongozi wa umma, zoezi ambalo
limeongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda.
Katika hatua nyingine, Rais wa Jamhuri yabMuungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli amekutana na kufanya
Mazungumzo na mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates ya
Marekani Bi. Melinda Gates ambapo Rais
Magufuli amemuhakikishia mwenyekiti
mwenza huyo kuwa serikali ya awamu ya
tano itaendeleza na kuimarisha zaidi
uhusiano wake na taasisi hiyo ambayo
imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Afya,
Uongozi na Kilimo.
Kwa upande wake Bi. Melinda Gate
amempongeza Rais Magufuli kwa kazi
kubwa anayoifanya katika kukabiliana na rushwa na kuongeza ukusanyaji wa mapato
ya serikali, na pia kwa nia yake thabiti ya
kuinua sekta ya kilimo inayotegemewa na
idadi kubwa ya watanzania na ameahidi
kuwa taasisi ya Bill and Melinda Gates
itaendelea kushirikiana na Serikali ya
awamu ya tano katika kuongeza tija ya
uzalishaji wa mazao ya kilimo.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, 


IKULU
Dar es salaam
29 Juni, 2016 .

Chapisha Maoni

 
Top