0
MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki
(Chadema), Tundu Lissu amewekwa rumande kwa
kukosa dhamana, mara baada ya mahojiano na
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam
kufuatia kauli yake aliyoitoa jana inayoelezwa
kuwa si ya kiungwana.
Mbunge huyo amehojiwa kwa saa tatu kuhusiana
na maneno mengine ambayo anadaiwa
kuyaandika kupitia mitandao ya kijamii kuwa ni
ya uchochezi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Kituo
cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam leo,
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekiri
kuwa Lissu amewekwa rumande kwa kukosa
dhamana na hataachiwa leo, hivyo atalala huko
mpaka kesho.

Chapisha Maoni

 
Top