wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo kuanzia
jana.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa
Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa ikimnukuu
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi
imesema Rais amemteua Dk Charles Mlingwa
ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Siha kujaza
nafasi hiyo.
Mulongo anakuwa mkuu wa mkoa wa pili
kutimuliwa kazi na Rais Magufuli baada ya Anne
Kilango Malecela aliyekuwa Shinyanga.
Hata hivyo, tofauti na Kilango ambaye alitimuliwa
kutokana na kutoa taarifa potofu kuhusu
watumishi hewa mkoani mwake, Ikulu haikutoa
sababu za kutenguliwa kwa uteuzi wa Mulongo.
Mulongo ameondolewa madarakani miezi sita
baada ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa
aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Dk
Faisal Issa baada ya kutofautiana na Mulongo
wakati huo akiwa mkuu wa mkoa huo.
Baada ya kumwondoa Dk Issa na nafasi yake
kujazwa na aliyekuwa Kamishna wa Polisi, Fedha
na Utawala (CP) Clodwig Mtweve, miezi miwili
baadaye Rais alimbadilisha Mulongo kituo cha
kazi akimhamishia Mara.
Alipoulizwa jana jinsi alivyoipokea hatua hiyo
iliyochukuliwa dhidi yake Mulongo alisema: “Sina
taarifa rasmi.”
Kabla kuhamishiwa Mara akitokea Mwanza,
Mulongo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Alishika nafasi hiyo baada ya kupandishwa cheo
akiwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo.
Chapisha Maoni