Mitatu mfululizo wamepoteza Fainali ya
Mashindano makubwa baada ya asubuhi hii
kubwagwa kwenye Fainali ya COPA AMERICA
CENTENARIO na Mabingwa Watetezi wa Copa
America Chile huko MetLife Stadium, New
Jersey, USA.
Mechi hii ilikwenda Dakika 120 baada ya Sare
ya 0-0 na kuamuliwa kwa Mikwaju ya Penati
Tano Tano kama ilivyokuwa kwenye Fainali ya
Copa America Mwaka Jana huko Santiago,
Chile na kama ilivyokuwa Mwaka Jana, Chile
walitoka tena kidedea kwa kuitungua
Argentina kwa Penati 4-2.
Hapo Kikosi cha Chile kikaibuka na Nyimbo:
"OYE, OYE, CHILE!"
Mwaka Juzi, Argentina walifungwa 1-0 na
Germany kwenye Fainali ya Kombe la Dunia
huko Brazil na kushindwa kwao Leo ni
mwendelezo wa Miaka 23 ya Argentina
kukosa Taji kubwa ambapo Staa wao
mkubwa, Lionel Messi, ambae ni Mchezaji
Bora Duniani mara 5, anaendeleza ukame wa
Taji kubwa na kuifanya Dunia ishindwe
kumweka ngazi ile ile ya Lejendari Diego
Maradona, alietwaa Kombe la Dunia mara 1
na Argentina, na Lejendari wa Brazil, Pele,
aklietwaa Kombe la Dunia mara 3 na Brazil.
Leo hii, kwenye Mikwaju ya Penati Tano Tano,
baada ya Chile kukosa Penati yao ya Kwanza
iliyopigwa Arturo Vidal na Kipa wa Man
United, Sergio Ramos, kuokoa, akaja Lionel
Messi na kupaisha juu Penati ya Kwanza ya
Argentina.
Penati zilizofuata zilifungwa na Castillo,
Aranguiz, Beausejour kwa Chile na Argentina
kufunga kupitia Mascherano na Sergio
Aguero na kufanya Penati ziwe 3-2 na ndipo
akaja Biglia wa Argentina na kupiga Penati
iliyodakwa na Kipa Claudio Bravo.
Chile wakafunga Penati yao ya 5 iliyopigwa
na Silva na kuwapa ushindi wa Penati 4-2.
Katika Dakika 90 za Mchezo, Mechi hii iliingia
dosari kwa Kadi Nyekundu 2 wakati kwenye
Dakika ya 28, Diaz wa Chile alipotolewa nje
kwa kumchezea Rafu Messi na kupewa Kadi
ya Njano ya Pili na hivyo kuonyeshwa Kadi
Nyekundu na katika Dakika ya 42 ikawa zamu
ya Argentina wakati Marcos Rojo alipopewa
Kadi Nyekundu moja kwa moja kwa
kumchezea Rafu Vidal.
Copa America inayofuata itachezwa huko
Brazil baada ya Miaka Mitatu.
VIKOSI VILIVYOANZA:
Argentina: Romero; Rojo, Otamendi, Funes
Mori, Mercado; Banega, Mascherano, Biglia;
Messi, Higuain, Di Maria
Chile: Bravo; Beausejour, Medel, Jara, Isla;
Vidal, Aranguiz, Diaz; Fuenzalida, Sanchez,
Vargas
REFA: Heber Roberto Lopes [Brazil]
COPA AMERICA
RATIBA/MATOKEO:
**Saa za Bongo
Robo Fainali
Ijumaa 17 Juni 2016
USA 2 Ecuador 1 [RF1]
Jumamosi 18 Juni 2016
Peru 0 Colombia 0 [Penati 2-4] [RF2]
Jumapili 19 Juni 2016
Argentina 4 Venezuela 1 [RF3]
Mexico 0 Chile 7 [RF4]
NUSU FAINALI
Jumatano 22 Juni 2016
USA 0 Argentina 4
Alhamisi 23 Juni 2016
Colombia 0 Chile 2 RF4
MSHINDI WA TATU
Jumapili 26 Juni 2016
USA 0 Colombia 1
FAINALI
Jumatatu 27 Juni 2016
Argentina 0 Chile 0 [Dakika 120, 0-0, Chile
Mabingwa Penati 4-2]
++++++++++++++++++++++++
DIBAJI:
Safari hii, Mashindano haya Copa América
Centenario ni mahsusi kusheherekea Miaka
100 ya Copa America, Mashindano ya
Shirikisho la Soka la Nchi za Marekani ya
Kusini, CONMEBOL, ambayo yalianzishwa
Mwaka 1916 na hii ni mara ya kwanza kwa
michuano hii kuchezwa nje ya Marekani ya
Kusini.
Haya ni Mashindano ya 45 kufanyika na
kawaida yake hufanyika kila baada ya Miaka
Minne lakini safari hii CONMEBOL na
CONCACAF, Shirikisho la Soka la Nchi za
Marekani ya Kaskazini, Kati na Nchi za Visiwa
vya Caribbean, walikubaliana kuandaa
Mashindano maalum.
Safari hii michuano hii itakuwa na Nchi 16,
badala ya 12 za kawaida, kwa kushirikisha
Nchi 10 kutoka CONMEBOL na 6 za
CONCACAF.
Kawaida Mshindi wa Copa America
huiwakilisha Marekani ya Kusini kwenye
Mashindano ya FIFA ya Kombe la Shirikisho
lakini Mshindi wa Copa América Centenario
hatapewa hilo kwani Mwaka Jana Chile,
wakiwa Nyumbani kwao, ndio walitwaa Copa
America ya kawaida na wao ndio watashiriki
Mashindano ya FIFA ya Kombe la Shirikisho
Mwakani, 2017, huko Russia.
Chapisha Maoni