JOHN MAGUFULI amewahimiza viongozi wa Baraza
Kuu la Waislamu Tanzania- BAKWATA- waendelee
kuombea amani katika taifa na kukemea ipasavyo
vitendo vya uhalifu katika jamii ya Kitanzania.
Kauli hiyo ya Rais imetolewa jana na Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA
SULUHU HASSAN kwa niaba ya Rais katika tafrija
ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania- BAKWATA- katika uwanja wa shule ya
sekondari ya KINONDONI MUSLIM jijini Dar es
Salaam.
Rais Magufuli amesema jamii yeyote inayolelewa
na kukua katika misingi ya kufuata maandiko ya
Mwenyezi Mungu ni vigumu kujiingiza kirahisi
katika vitendo vinavyomchukiza Mungu vikiwemo
vitendo vya uhalifu.
Rais MAGUFULI pia amewatakia kheri waumini
wote wa dini ya kiislamu kote nchini katika mfungo
wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Kwa upande wake, Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh
ABUBAKAR ZUBEIR ameipongeza serikali kwa
hatua inazochukua katika kukabiliana na vitendo
vya uhalifu hapa nchini na kusisisita kuwa
Viongozi wa BAKWATA na wataendelea
kushirikiana na serikali katika kukemea vitendo
viovu katika jamii kama hatua ya kuhakikisha
vitendo vya uhalifu vinakoma hapa nchini.
Mufti wa Tanzania pia ametoa rai kwa waislamu
wote nchini wadumishe umoja,upendo na
mshikamano miongoni mwao katika Mfungo wa
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na hata baada ya
mfungo kama kitabu kitukufu cha QUR’AN
kinavyoelekeza.

Chapisha Maoni