karatasi ya kuiomba nchi yao kuridhia kurudiwa
tena kwa kura ya maoni itakayotoa maamuzi kama
nchi hiyo iendelee kubaki katika Umoja wan chi za
ULAYA au kujitoa.
Tayari kura ya maoni iliyopigwa nchini humo siku
ya Ijumaa, iliamua kuwa UINGEREZA ijitoe kwenye
Umoja wan chi za ULAYA.
Wanaharakati mbalimbali wamekuwa wakikusanya
saini, baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya
wananchi wa UINGEREZA yaliyofanywa mwishoni
mwa wiki iliyopita.
Wanaharakati hao awali waliiomba serikali ya
UINGEREZA, kuridhia kurudiwa kwa kura hiyo
endapo asilimia ndogo ya watu wataridhia nchi yao
kujitoa ikizingatiwa kuwa ni asilimia 75 peke yake
ya wananchi ndio walijitokeza kupiga kura.
Kwa mujibu wa matokeo hayo asilimia 52 ya
wananchi wa UINGEREZA ndio wanataka serikali
yao kujitoa kwenye Umoja huo. Watu hao
wanasema kuna hasara kubwa endapo UINGEREZA,
itajitoa kwenye Umoja wan chi za ULAYA.
Wakati huo huo Kansela wa UJERUMANI, ANGELA
MARKEL, amesema hakuna haja ya kurushiana
maneno mabaya kati ya wananchi wa UINGEREZA,
serikali yao pamoja na nchi nyingine za Umoja wa
ULAYA, baada ya wananchi kuamua nchi hiyo
kujitoa kwenye Umoja huo.
ANGELE amesema, bado mazungumzo ya
kibiashara yanaweza kufanyika baina ya pande
hizo mbili, na hali ya maelewano ikaendelea
kuwepo, bila kelele.
TBC
Chapisha Maoni