0
Siku chache tu baada ya Uingereza kupiga kura ya
kujiondoa kwenye muungano wa ulaya, sarafu ya
nchi hiyo imeendelea kudorora mapema leo katika
soko la ubadilishanaji wa fedha.
Baadhi ya masoko ya hisa katika bara la Asia
yameanza kuimarika kufuatia kuporomoka kwa
paundi kuanzia Ijumaa iliyopita.
Waziri wa fedha wa Uingereza, bwana George
Osborne, amezihakikishia masoko ya Ulaya kuhusu
matumaini ya siku zijazo kufuatia kura hiyo ya
kujitenga.
Soko la ubadilishanji wa fedha limefunguliwa leo
likiwa asilimia 0.8% chini ya kiwango
kilichoshuhudiwa ijumaa.
Kigezo cha Soko la hisa la FTSE lilifunguliwa leo
likiwa na pointi 6,092.19.
Pauni ya Uingereza ilibadilishwa na dola $1.3463,
za marekani ikiwa ni asilimia 2% chini ya kiwango
cha Ijumaa.
Dhidi ya sarafu ya Ulaya Euro inabadilishwa na
€1.2170,ikiwa ni asilimia 1.2% chini ya kiwango
cha ijumaa.
Waziri wa fedha bwana Osborne amesema kuwa
uchumi wa Uingereza utalazimika kujifunga
kibwebwe kwani waingereza watalazimika kusubiri
kwa muda kuteuliwa kwa waziri mkuu mpya
atakayetoa mwelekeo mwafaka wa taifa.
Huko Asia , serikali zimekuwa zikisaidia soko la
ubadilishanaji wa fedha zisiporomoke zaidi na
kuathiri vibaya uchumi wa eneo hilo.
BBC

Chapisha Maoni

 
Top