ya ndege yaliyopatikana ufuoni, Pemba ni ya
ndege ya Malaysia iliyotoweka miaka miwili
iliyopita.
Picha za mabaki hayo yaliyopatikana visiwa vya
Pemba zimekuwa zikisambaa sana mtandaoni
tangu juzi.
Maafisa wa Tanzania wamewasiliana na maafisa wa
Malaysia ambao wanapanga kutuma wachunguzi.
Hilo litawezekana tu wakati watengenezaji wa
ndege hiyo watafika na kuchunguza mabaki hayo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uchukuzi wa Ndege
Tanzania Redemptus Bugomola ameambia BBC
kwamba bado ni mapema mno kubaini iwapo
mabaki hayo ni ya ndege ya MH370.
Shirika la habari nchini Malaysia Bernama
lilimnukuu waziri uchukuzi nchini humo Liow
Tiong Lai, akisema kuwa mabaki ya ndege hiyo
yatafanyiwa uchunguzi kubainia ikiwa yana
uhusiano na ndege ya Malaysia iliyopotea ya
MH370.
"Mabaki hayo ya ndege ni makubwa ... lakini ni
baada tu ya kubaini kwamba ni ya ndege aina ya
Boeing 777 ndipo tutatuma wachunguzi huko
kwenda kuchunguza iwapo kweli ni ya MH370 au
la," amesema Liow.
Ndege hiyo ya Boeing 777 nambari MH370
ilitoweka 2014 ikiwa na watu 239 muda mfupi
baada ya kupaa kutoka Kuala Lumpur ikielekea
Beijing.
Vipande vya ndege hiyo vilipatikana katika visiwa
vya Reunion Julai mwaka 2015.
Hivi majuzi, mabaki ya ndege sawa na hiyo
yalipatikana Madagascar lakini baada ya uchunguzi
ikabainishwa kwamba hayakuwa ya ndege hiyo ya
MH370.
Chapisha Maoni