Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kimewasili jana
usiku tayari kwa mchezo dhidi ya Yanga hapo
kesho Jumane Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Mara baada ya kuwasili, mshambuliaji Mtanzania
anayecheza katika klabu hiyo Thomas Ulimwengu
ambaye muda mwingi alikuwa akionyesha ishara
ya vidole vitatu amesema, wanajua wamekuja
kucheza na timu bora na wanaiheshimu Yanga
lakini watapambana ili kuweza kushinda katika
mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri
ya kwenda fainali.
Ulimwengu amesema, anaifahamu Yanga na
wachezaji wake wengi ambao yupo nao timu ya
taifa ya Tanzania na anaamini mchezo utakuwa
mgumu.
Mabingwa hao mara tano wa Afrika watamenyana
na Yanga katika mchezo wa Kundi A Kombe la
Shirikisho Afrika Jumanne katika Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Mazembe imekuja na kikosi cha wachezaji 18
ambao ni; Robert Kidiaba, Sylvain Gbohou, Issama
Mpeko, Joel Kimwaki, Thomas Ulimwengu,
Christian Koume,
Jean Kasusula, Salif Coullbaly, Merveille Bope,Jose
Badibake, Kissi Boateng, Roger Assale, Rainford
Kalaba, Deo Kanda, Adama Traore, Chriastian
Luyindama, Nathan Sinkala na Joas Sakuwaha.
Maofisa wa benchi la Ufundi wanaokuja ni
Theobald Binamungu, Mohamed Kamwanya,Dony
Kabongo, Frederic Kitengie na Andre Ntime.
Madaktari ni Hurbert Velud, Pamphile Mihayo,
Mhudumu Richard Mubemb na Maofisa wa Idara ya
Habari na Mawasiliano, Heritier Yinduka, Arther
Kikuni na Meshack Kayembe.
Chapisha Maoni