0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles
Mwijage ameeleza mpango wa kufufua kiwanda
cha kutengeneza matairi ya magari cha General
Tyre, kwa kununua mashine mpya za kisasa.
Mwijage hivi karibuni alitangaza kuwa baada ya
miaka mitano mtu atakayevaa nguo kutoka nje
azomewe mitaani, kwani viwanda vya ndani
vitakuwa vimeanza uzalishaji.
Akizungumza mkoani Arusha jana, Mwijage
alisema wataalamu wametumwa nje ya nchi
kufanya utafiti wa mashine mpya za kutengeneza
matairi.
Naye Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema
aliitaka Serikali kuharakisha kukifufua kiwanda
hicho, kwani kina uwezo wa kutoa ajira nyingi kwa
vijana.
Mwananchi

Chapisha Maoni

 
Top