0

Zlatan Ibrahimovic, 34, atasaini mkataba wa mwaka
mmoja Manchester United siku ya Ijumaa.
Mchezaji huyo pia atapewa kitita cha pauni milioni
4 kama bakshishi ya ‘uzalendo’ kutoka PSG
(Gianluca Di Marzio), AC Milan wanakaribia kuuza
hisa kiasi kubwa kwa kundi la wawekezaji kutoka
China ambao wanataka kumsajili mshambuliaji wa
Everton Romelu Lukaku, 23 (Gazzetta dello Sport),
meneja wa Arsenal, Arsene Wenger atakutana na
wawakilishi wa mshambuliaji wa Ufaransa na Lyon,
Alexandre Lacazette, 25, anayedhaniwa kuwa na
thamani ya pauni milioni 45 (Sun), Leicester City
wanazungumza na Norwich kutaka kumsajili winga
Robbie Brady, 24 (Leicester Mercury), beki kutoka
Serbia Neven Subotic, 27, aliyenunuliwa na Jurgen
Klopp alipokuwa Borussia Dortmund amethibitisha
kuwa anataka kuondoka katika klabu hiyo (Daily
Express), Chelsea watapanda dau kwa mara ya tatu
kumtaka kiungo wa Roma Radja Nainggolan wiki
hii na pia kiungo wa Leicester N’Golo Kante, 25
(Daily Mirror), Southampton wanapanga
kumtangaza Mfaransa Claude Puel kuwa meneja
mpya wiki hii (Daily Telegraph), mshambuliaji wa
Spain na Celta Vigo, Nolito, 29, amesema anasikia
fahari kuhusishwa na Manchester City na
Barcelona, lakini kwa sasa anafikiria michuano ya
Euro 2016 (La Vanguardia), Borussia Dortmund
wamepanda dau kumtaka mshambuliaji wa Bayer
Leverkusen Karim Bellarabi, 26, kwa kuwa
wanatarajia kuondoka kwa Henrikh Mkhitaryan, 27,
anayedhaniwa kwenda Manchester United (Daily
Mirror), uhamisho wa Mkhitaryan kwenda Old
Trafford unakaribia kukamilika baada ya maafisa wa
Dortmund kwenda Manchester kuzungumzia dau la
United kwa kiungo huyo kutoka Armenia (Sun),
Paris St-Germain wanamnyatia kiungo wa Sevilla
Grzegorz Krychowiak, 26, na wako tayari kulipa
pauni milioni 32 (Marca), beki wa Barcelona Dani
Alves, 33, anakaribia kuhamia Juventus na huenda
akafanya vipimo vya afya siku ya Jumatatu
(Goal.com ). 

Chapisha Maoni

 
Top