0
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East AFrica
Radio, TID amesema Dully Sykes hakupenda
kitendo cha Joh Makini kuwepo kwenye
collabo yao ya wimbo wa confidence.
“Kwanza ile ngoma mwenyewe ndio alitaka
kuwepo baada ya kuisikia, akasema mnyama
hii ngoma kali naomba niweke sauti na mimi,
nikamkubalia tukarekodi, lakini alivyokuja
kusikia Joh Makini yupo akanipigia simu tena
usiku, akaanza kunifokea, tena imagine ngoma
yangu ananifokea..TID vp unaweka watoto wa
Arusha? ndo unafanya nini?” , alisema TID,
TID aliendelea kwa kusema kuwa licha ya hilo
baada ya kuandaa show ya ku-launch audio,
alivyoona na Joh Makini anaperfom, akampigia
Joh akimwambia asikubali kufanya show bila
kumlipa.
“Baada ya hapo akampigia Joh akamwambia
Joh ile show kubwa usikubali kuperfom bila
kukupa milioni tatu, baadaye Joh akaniambia
kwamba bila mkwanja haparfom, nikamuuliza
we habari hizo umezitoa wapi? akaniambia ni
Dully kanambia, nikamwambia ungejua huyo
Dully alimind kusikia we upo kwenye ngoma!
bahati nzuri siku Dully ananipigia kina
nNicotrak walisikia”, alisema TID.
TID aliendelea kusema kuwa Dully ana mambo
ya kitoto hivyo anahitaji kuacha ushindani
usiokuwa na faida, na kushindana kikazi.

Chapisha Maoni

 
Top