0
Uongozi wa Yanga umesema kuwa haujaridhishwa
na vitendo vya hujuma wanavyofanyiwa na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF kwa
kuingia mikataba ambayo haitakuwa na faida kwa
klabu hiyo pamoja na kutumia nafasi yao vibaya
kwa kuwasiliana na Shirikisho la Soka Barani
Afrika CAF bila kuwashirika na kuwadanganya, hilo
limekuja baada ya TFF kusaini mkataba wa
kurusha matangazo ya mpira na kampuni ya Azam
bila wao kushirikishwa na kusema kuwa suala hilo
hawatalifumbia macho.
Akitoa ufafanuzi kuhusiana na suala hilo, Mkuu wa
Kitengo cha habari na Mawasiliano wa Yanga,
Jerry Muro amesema Yanga hawakatai mechi
kuonyeshwa ila Kitendo cha TFF kuingia mkataba
pasipo Yanga kujua na wakatuma taarifa CAF kuwa
wamekubaliana katika haki ya matangazo kitu
ambacho si cha kweli na hawajapendezewa nacho
na kwahilo hawatakaa kimya kwani wana uhakika
kuwa wana nia mbaya ya kuijuhumu timu yao.
Kama wanataka kuonekana kwa mechi hiyo basi
wanatakiwe wakae na kuzungumza la sivyo
watakwenda mbele zaidi.
"TFF na Azam wamekosea na kama hawatataka
kukaa pamoja na kuliongelea suala hili basi
hatutakaa kimya bali tutaenda mbele zaidi kwani
inaonyesha dhahiri ni vitendo vya rushwa
vinavyoendelea ndani ya mpira,"amesema Muro.
Wakati huo huo Yanga imetaja viingilio viwili tu
katika mchezo wake wa Kundi A Kombe la
Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DRC
Jumanne Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari makao
makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam mchana
wa leo, Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano ya
Yanga, Jerry Muro amesema viingilio hivyo ni Sh.
7000 kwa majukwaa ya mzunguko na Sh. 30,000
kwa VIP.
Muro amesema tiketi zitaanza kuuzwa Jumatatu
mjini Dar es Salaam kuelekea mchezo huo ambao
utaanza Saa 10:00 jioni Jumanne ijayo.

Chapisha Maoni

 
Top