kwenye boti wakitokea Mitomoni, wilaya ya
Songea Vijinini, mkoani Ruvuma kwenda mnadani
katika wilaya hiyo wanahofiwa kufa maji baada ya
boti hiyo kuzama kwenye Mto Ruvuma.
Habari zilizopatikana jana mjini hapa zilieza kuwa,
boti hiyo ilikuwa imejaza abiria pamoja na mizigo
iliyokuwa ikipekwa kwenye mnada wa hadhara
ambao upo jirani na kijiji cha Mitomoni mpakani
mwa Tanzania na Msumbiji.
Jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, hazikufanikiwa
baada ya kuelezwa kuwa alikuwa ameungana na
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma
kwenda kwenye eneo la tukio hilo.
Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa
Ruvuma, Hamis Kutiku, alisema Kamanda
Mwombeji amekwenda kwenye eneo la tukio ili
kujiridhisha ukweli wa tukio hilo.
Alisema taarifa kamili juu ya tukio hilo zitatolewa
baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama kufika
eneo la tukio na kurudi mjini kwa ajili ya hatua
zaidi kuchukuliwa.

Chapisha Maoni