0
MWILI wa Mbunge wa zamani wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM), unatarajiwa kuzikwa Alhamis wiki hii.
Taarifa iliyotolewa jana na kaka wa marehemu,
Enock Madimilo, ilisema taratibu za mazishi
zinaendelea kufanywa nyumbani kwa marehemu
Dar as Salaam na Arusha.
“Tunaendelea na mipango ya mazishi hapa
Arusha na nyumbani kwa marehemu, Ada Estate
jijini Dar es Salaam.
“Mazishi yatafanyika hapa Arusha Alhamisi wii hii.
Kwa hiyo, tunawaomba ndugu, jamaa na marafiki
wa marehemu, waje kumuaga mpendwa na
kiongozi wao,” alisema Madimilo.
Shelukindo alifariki juzi usiku saa 2:30 akiwa
nyumbani kwa mama yake mzazi, katika eneo la
Olorien, jijini Arusha baada ya kuugua kwa muda
mrefu.
Mwili wa marehemu Beatrice uliondolewa
nyumbani kwa mama yake huyo alipokuwa
akiuguzwa usiku huo huo na kupelekwa Hospitali
ya Mount Meru.
Kutokana na msiba huo, tayari waombolezaji
mbalimbali wameendelea kufika nyumbani kwa
mama wa marehemu kwa ajili ya kutoa pole.

Chapisha Maoni

 
Top