Mwanamuziki mkongwe kwenye muziki wa bongo fleva Afande Sele amefunguka na kusema kwa sasa anajisikia kuoa tena baada ya muda
mrefu kupita akiishi mwenyewe na kutofurahia maisha anayoishi kutokana na kukosa mke.
Afande Sele siku kadhaa zilizopita alisema kuwa
yupo na marafiki kadhaa wa kike ambao
wanamsaidia kulea watoto wake, na kumfanya
aishi akiwa na amani kwani wanamsaidia kutunza watoto, na kudai ya kwamba yeye anaona wanachunguzana na hao mabinti ili
akiona yupo mmoja wapo ambaye ana sifa ya
kuwa mke bora aweze kuwa naye kama malkia kwa kuwa yeye ni mfalme.
Lakini leo kupitia ukurasa wake wa Facebook
aliweka picha akiwa anakula chakula kwenye sufuria na kutoa sababu ambazo zinamfanya
atamani kuoa tena, moja wapo ni uvivu wa kuosha vyombo ndiyo maana anaamua kula kwenye sufuria.
“Najisikia “kuoa” tena…Mara chache huamua kula
kwenye sufuria kwa sababu naishi mwenyewe hivyo napika mwenyewe, naosha vyombo
mwenyewe nk, hivyo kwasababu ya uvivu wangu
katika kuosha vyombo wakati flani huamua kula kwenye sufuria ili kuepuka kuchafua vyombo,
zaidi pasi na ulazima’anko magu style'” aliandika Afande Sele
eatv.tv
Chapisha Maoni