0
Nyota wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, anatarajia kukata rufaa ya
kifungo chake cha kwenda jela miezi 21 kwa kosa
la udanganyifu wakati wa ulipaji kodi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 na baba yake wanadaiwa kukwepa kulipa kodi ya mwaka
2007 na 2009, kwa ajili ya matangazo ya picha za mchezaji huyo.

Fedha za matangazo hayo zilikuwa zinakusanywa
na baba yake na kuzipeleka mafichoni kwenye visiwa vya Belize na nchini Uruguay ambapo
hakuna makato ya kodi.
Kutokana na hali hiyo mchezaji huyo na baba yake walishtakiwa na juzi walihukumiwa kwenda jela
miezi 21 na kutakiwa kulipa faini jumla ya pauni milioni 4.9.
Hata hivyo, Sheria za mahakama nchini Hispania, zinasema mshtakiwa ambaye anatakiwa kutumikia
jela chini ya miaka miwili anaweza kuwa chini ya
uangalizi, hivyo Messi na baba yake wanaweza wasitumikie gerezani wakatumikia kifungo cha nje
na kulipa faini hiyo.
Mwanasheria wa mchezaji huyo na baba yake amesema kwamba, wanatarajia kukata rufaa juu ya
kesi ya mteja wake.
Mwanasheria huyo amedai watapambana kwa hali
na mali kuhakikisha mchezaji huyo anakuwa huru
na anaendelea kucheza soka lake.
Kitendo hiki kinaweza kumweka katika wakati
mgumu mchezaji huyo hasa kwenye msimu mpya
wa ligi, kutokana na ujumbe ambao anaupata mara
baada ya kutangaza kujiuzulu kuitumikia timu ya taifa.

Chapisha Maoni

 
Top